CHOBA
TZS 15,000
-
Pages
Pdf
Format
Lifetime
Access
0
Sales
Description
Kisa cha Kijana Choba ni hadithi ya kuonesha jinsi maishaduniani hapa yawezavyo kumbadilikia mtu katika kuishi
kwake. Anaanza kwa shida kwa sababu ya uhasama wa watu
wengine, Lakini Mungu mweza yote anambadilishia maisha na
kujikuta amekuwa tajiri bila kujua.
Choba na Bonge walikuwa watu wa damu moja lakini
hawakufahamiana hadi mwisho katika harusi ya Choba. Mzee
Juma aliishi kwa shida baada ya Mkewe na mtoto kumtoroka na
kumwacha peke yake. Lakini bila kujua akamkarimu Choba
alipokuwa kwenye hali ya ufukara mkubwa. Wawili hawa
wakakutana na Bonge aliyewahisani na kuwafanya matajiri.
Ma Jesca na bintiye wakarudi kwa Mzee Juma baada ya kuona
kumenoga. Kijana Choba hakukawia kuona, Umama wa
nyumbani, kwa Jesca. Bila kukawia akawahisha barua ya posa
ambayo ilipokelewa na kukubaliwa. Hata hivyo mambo ya posa
na mahari yalipigwa Stop hadi kumaliza masomo yaliyotakiwa ili
waweze kupokea ajira katika Kiwanda cha CHOBEMICO.
Jesca na Choba walipokuwa masomoni Canada hawakutetereka
katika mahusiano. Walijiweka katika hali ya utawa hadi
waliporudi nyumbani na kufunga ndoa katika harusi iliyofana .
Hili ni somo kwa vijana wa leo wanapokuwa chuoni wazingatie
masomo ili kuepuka hali ya mapenzi na kujamiana ambavyo
huwaletea madhara. Kujamiana ni heshima ya watu walio
kwenye ndoa. Nje ya hapo unakuwa umetenda dhambi mbele ya
Mungu, kwa wazazi na jamii pia.
About the Author
Customer Reviews
No reviews yet. Be the first to review!