HABARIDUKA - Tanzanian Digital Marketplace
Back to Story
Nyota Ya Mrembo Aliyezikwa Hai - Chapter 3: Siri Zinapoanza Kuvuja

Nyota Ya Mrembo Aliyezikwa Hai - Chapter 3: Siri Zinapoanza Kuvuja

Kila alichojaribu kufanya Peter kujiondoa kwenye hali ile kilishindika. Isingekuwa Janeth ni mwanamke wa jamaa yake basi asiwaza muda mrefu vile angeshakuwa kamaliza mchezo mapema kabisa.

Peter: Shem, basi...(kabla hajamaliza alichotaka kusema Janeth alimkatisha).

Janeth: Aah Peter na wewe acha kuniita Shem bwana (alisema kwa sauti ya mideko).

Peter: Aah! Basi Janeth tafadhali wacha niende chooni kwanza nikojoe.

Janeth: Aya fanya haraka basi kabla hamu haijakata.

Janeth alitoka juu ya Peter na moja kwa moja kuelekea uani. Akiwa huko alibaki kujiangalia kwenye kioo ni nini hiki anafanya? Huyu si shemeji yake? Alisimama akijiangalia kwenye kioo na kujiuliza hayo maswali.

"Aah! potelea pote bwana, Johnson mwenyewe huwa yuko mbali mno muda mwingi." Peter alijisemesha kwa sauti. Akatoka kule chooni na kuanza kurudi kuelekea pale sebleni ambako sasa alikuta Janeth amebaki mtupu katoa hata kile kijora alikuwa amevaa.

Peter alisimama kama mtu aliyepigwa na butwaa alipoona ule mwili wa Janeth. Mrembo mweupe asiye na doa hata moja kwenye ngozi yake. Umbo lake ni kama mavazi alipendelea kuvaa mara kwa mara hayakuwa yanamtendea haki. Umbo namba nane kabisa na huyu mrembo alikuwa analificha kwa kuvalia nguo zisizoonesha umbo hili vizuri. Mtoto mashallah kabisa kama vile aliumbwa na Mungu siku Mungu akiwa mapumziko na alimuumba akiwa ametulia.

Kwa macho ya ushawishi yakiwa yamelegea mikono ikichezea matiti yake mwenyewe, mrembo Janeth alimuita Peter kwa sauti ya mahaba mno, "Baby njoo bwana mimi nina hamu na wewe."

Janeth alijua haswa kutumia uzuri wake kushawishi mwanaume. Mpaka Peter alijiuliza kama kweli huyu ni mchaga. Isije kuwa ni binti wa Tanga huko amekuja mjini kutudanganya yeye ni mchaga.

Polepole Peter anaanza kusogea kumfuata Janeth huku tayari ameanza kufungua vifungo vya juu vya shati lake. Anamsogelea kabisa Janeth na kuanza kumbusu kwenye midomo yake polepole.

Janeth: Subiri kwanza nikae vizuri naumia.

Peter: (kimya bila kusema chochote anasimama ili Janeth akae vizuri).

Ghafla simu ya Janeth pale mezani inaanza kuita na jina linasoma "Mme Wangu" na picha ya Johnson. Peter alitoka mbio kama vile ameitiwa mwizi. Alisahau hata ambacho walianza kufanya pale.

Haraka sana aliwasha pikipiki yake na kuanza kuondoka mahali pale. Walinzi kama tunavyowajua na kazi yao kuwataka kuwa wambea anamsimamisha Peter pale getini.

Mlinzi: Boss vipi bwana kuna usalama.

Peter: We bwana hebu fungua geti niende zangu mimi.

Mlinzi: Mbona jasho nyingi hivyo. Huko ndani umemuacha dada salama? Au umemdhuru?

Peter: Mama mwenye nyumba wako yuko salama ndani hapo nenda wewe mwenyewe kamuangalie.

Mlinzi: Aah! Boss tuongee kiustaarabu tu kama mwanzo ilivyokuwa.

Peter: Pisha nifungue mwenyewe kama hutaki.

Mlinzi huyo mbio kuelekea kwenye nyumba. Haraka nae kaingia moja kwa moja maana mlango ulikuwa wazi. Anakuta Janeth kasimama pale sebleni akiwa bado mtupu na simu iko sikioni.

Janeth: Wewe unafata nini huku?

Mlinzi: Aah samahani Boss nilikuja kuangalia kama uko salama.

Janeth: Hebu toka hapa.

Mlinzi wa watu akageuka haraka na kuondoka. Aliondoka akiwa na aibu na wasiwasi wa kupoteza kazi yake. Pale nje Peter tayari alishafungua geti na kuondoka zake.

Huku ndani Janeth aliendelea na mazungumzo kwenye simu.

Janeth: Samahani baba angu, mlinzi wako huyu kaingia tu ndani bila kugonga hodi.

Johnson: Alikuwa anataka nini?

Johnson japokuwa ni mtu mwenye hasira ila hakuwahi kukurupuka kupiga kelele wala kuwa mkali bila sababu.

Janeth: Aah! Sijui hata anataka nimemtimua mimi, maana nimejikalisha tu sebleni hapa na sijavaa kitu.

Johnson: Ooh! pole mamii. Ila hebu jitahidi uwe unavaa mara nyingi nakwambia.

Janeth: Sasa baby nipo kwangu ila bado nivae manguo? Kuna haja gani sasa ya kuwa kwangu?

Johnson: Aah! basi yaishe mama angu. Kama kila kitu kipo sawa basi mimi nikuage niendelee na kazi.

Janeth: Sawa mpenzi uwe na wakati mwema, ngoja nikavae mara moja niende kule dukani kuchukua mauzo.

Johnson: Alafu nikirudi tutazungumza kuhusu suala la wewe na kazi yako.

Janeth: Sawa babaa.

Janeth akaenda kujiandaa ili aende zake dukani kwake kufunga hesabu zake. Wakati anatoka getini alimuangalia mlinzi kwa jicho la hasira na akafyonya sana.

Masikini mlinzi wa watu bila kosa lolote alianza kuchukiwa na Boss ambaye mwanzo alimjali sana. Janeth hakuwa kumchukia huyu mlinzi. Ikiwa mlinzi ana shida na pesa au chochote kile Janeth hakusita kumsaidia. Kuna kipindi mlinzi alikosa hata ada ya mwanae shuleni, Janeth ndiye alilipa. Pamoja na mapungufu yake yote Janeth ni mtu aliwajali sana watu wasio na uwezo.

Basi mlinzi alifunga geti lake baada ya Boss wake kutoka na akaendelea na kazi zake. Haukupita muda mrefu sana kabla simu yake ianze kuita. Ni Johnson alipiga simu.

Mlinzi: Haloo Boss, heshima yako mkuu.

Johnson: Unaendeleaje bwana Maiko?

Mlinzi Maiko: Kwema Boss wangu sijui wewe huko.

Johnson: Huku salama. Vipi hapo nyumbani kila kitu kipo sawa?

Maiko: Ndiyo Boss hapa kuko salama, ila samahani Boss leo nimekosea jambo hapa nyumbani.

Johnson: Nadhani hicho ndicho nilitaka zungumza na wewe.

Maiko: Tafadhali Boss naomba usinifukuze kazi sina mahali pengine pakutafutia kipato.

Johnson: Wala hatufiki huko. Mimi nataka tu uniambie nini haswa kimetokea siku ya leo hapo. Dada yako simuelewi kabisa leo.

Maiko: Boss samahani, lakini sidhani kama hiyo ni nafasi yangu kusemea maisha binafsi ya dada.

Johnson: Maiko kazi yako hapo ni kuhakikisha usalama, na ninapoona mambo hayako sawa na husemi nitakufukuza kazi kweli.

Maiko: Aah! samahani Boss basi ngoja nikwambie kila kitu.

Johnson: Aya niambie mara moja.

Basi Maiko bila kuacha hata punje ya mchele, alianza kusimulia yale yote yametokea. Kuanzi muda Janeth ametoka nyumbani mpaka aliporudi akiwa mwekundu na kajawa mawazo na hasira. Akaeleza namna Peter alikuja na kuondoka na namna alimkuta Janeth pale sebuleni na mpaka Janeth alipotoka tena. Baada ya kusema yote Johnson akauliza.

Johnson: Maiko unadhani nini kimetokea kati ya Peter na dada yako?

Maiko: Kiukweli Boss mimi sifahamu na siwezi sema chochote kuhusu yaliyotokea ndani.

Johnson: Okay! haina shida wewe endelea na kazi yako. Usimwambie shemeji yako kwamba tumezungumza. Endelea na kazi yako kama kawaida.

Maiko: Sawa, asante Boss wangu.

Johnson: Pia sasa hivi uwe unaniambia kila kitu kabla sijauliza. Muda anatoka na nani anakuja hapo nyumbani.

Maiko: Sawa boss nimekuelewa.

Baada ya kukata simu Johnson alikaa dakika kadhaa kimya akifikiria. Afanye nini kuhusu hawa watu wawili? Awache wamalize kabisa ili nae aendelea na mipango yake? Au awazuie wasiendelee ili amuokoe rafiki yake Peter?

Akaona isiwe tabu wacha kwanza ampigie Peter pia aone atasema nini.

Peter: Haloo Boss kwema?

Johnson: Aah! ndugu yangu nini na wewe unaniita Boss na hukuwahi kuniita hivyo.

Peter: (Kwa kigugumizi na wasiwasi anasema) Ha...Ham... Hamna kitu ndugu yangu si unajua tena kupitiwa. Vipi kuna habari gani?

Johnson: Nimeona kimya imebidi nikupigie. Shemeji yako anaendeleaje?

Peter hakujibu chochote maana moyo ulizidi kumuenda mbio na akawa haelewi kabisa kinachoendelea.

JohNson: Oya we Peter. Vipi mbona huongei?

Peter: Aah, pole ni mtandao unazingua (ilibidi ajitetee kuhusu mtandao)

Peter: Nilienda bwana. Yuko salama anasema alikuwa tu mbali na simu ila yuko safi kabisa.

Johnson: Na hakuna kitu kingine umeona?

Peter: Hakuna kaka, kwani vipi kuna usalama?

Johnson: Hakuna shida bro. Basi sawa shukrani wacha niendelee na kazi huku.

Simu ilikatwa bila kusubiri majibu ya Peter. Peter alianza kuwaza imekuaje tena au kuna kitu jamaa amejua au kuhisi kuhusu yale yametokea pale kwa Janeth?

Johnson akaona basi ni vyema kwamba hata rafiki yake ana nia ovu na yeye haina shida. Akafungua sehemu ya kutuma meseji kwenye simu yake na kuandika, "Shikamoo mtaalamu. Nadhani mpango wetu utatimia hivi karibuni. Kuna kijana mwingine tunaweza kumpata hivi karibu kupitia mwanamke yule yule."

Akarudisha simu mfukoni. Hazikupita dakika chache kabla simu yake ianze kuita. Yule mtaalamu aliamua kupiga.

Johnson: Mtaalamu sikutegemea ungeweza zungumza na simu muda huu.

Mtaalamu: Usijali kijana wangu, leo ni siku ya kupumzika, mizimu huwa imenipa siku mbili za mapumziko.

Johnson: Kumbe hata nyie mnapumzika?

Mtaalamu: Kupumzika muhimu kijana wangu, hata mizimu inahitaji muda kukusanya nguvu na upya.

Johnson: Anha! sawa sawa. Umeona ujumbe wangu.

Mtaalamu: Ndiyo nimeuona. Nilitegemea ungenitafuta mapema zaidi, lakini huyu rafiki yako amejitahidi sana kuvumilia mpaka sasa.

Johnson: Umejuaje kama ni rafiki yangu?

Mtaalamu: Haya mambo sisi tunayajua tu. Ikifika muda na wewe utafahamu.

Johnson: Hahahaha! Sawa mtaalamu. Hapa tayari tunaye yule kijana wa chuo na sasa huyu rafiki tukibahatika ataongezeka.

Mtaalamu: Ndiyo si muda sana tutamaliza yote. Usirudi nyumbani mpaka siku nikwambie. Mambo yakiwa tayari kabisa kati ya mpenzi wako na huyu rafiki yako nitakwambia.

Johnson: Anha sawa sawa mtaalamu tutaendelea kuwasiliana.

Huyu ndiye mtaalamu aliyefanya Johnson akawa na mafanikio makubwa sana kwa kipindi kifupi na kuwa na maisha bora. Johnson alikutanishwa na huyu mganga wa jadi na kigogo mmoja wakiwa semina moja ya madini pale Geita.

Johnson aliambiwa yeye hana nyota ya mafanikio ila atafute mwanamke mmoja mpambanaji mwenye shida na pesa na awe mpenzi wake. Huyu mwanamke ahakikishe ana nyota ya mvuto.

Basi kama bahati kuna siku Johnson akiwa kwenye mizunguko yake akakutana na Janeth kwenye duka moja la vyombo. Janeth alikuwa kaajiriwa katika lile duka kwa mshahara wa laki mbili tu kwa mwezi.

Johnson alivutiwa nae, ila alipokumbuka yale aliyoambiwa akaona labda hatafaa. Aliondoka zake na kuendelea na mambo yake. Siku nyingine tena aliorudi alikutana nae tena kwenye lile duka. Hapo akaona hapana leo lazima azungumze vyema na huyu mrembo.

Janeth alikpenda sana kusali, lakini ugumu wa maisha ulimfanya mara kwa mara ajikute anakuwa mdangaji. Janeth na Johnson walibadilishana namba za simu na kuanza tumia text mara kwa mara wakizidi kufahamiana. Baada ya kuzidi kumjua Janeth, Johnson akaona huyu binti anafaa.

Basi akarudi na kumwambia yule mganga kwamba kapata mwanamke sahihi. Mganga kwa njia zake na mizimu yake wakaangalia na kuona kweli binti huyu anafaa.

Basi kwa mara ya kwanza Johnson alipewa dawa za kienyeji na kupewa maelekezo kwamba, ajitahidi aanze kuishi na Janeth ndani ya miezi miwili ya mahusiano yao. Mwezi wa tatu unapofika siku ambayo Janeth ataingia hedhi, itabidi Johnson aweke dawa hizo kwenye chakula ambacho atakula Janeth. Juu ya hilo zile pedi ambazo Janeth atatoa akishatumia ahakikishe zinamfikia huyu mganga.

Johnson alijitahidi kufanikisha kumshawishi Janeth akaishi nae. Ajabu ni kwamba hata haikuwa ngumu. Janeth alipofika tu nyumbani kwa Johnson kwa mara ya kwanza alishawishika kuendelea kuishi nae hapo.

Aliona kama maombi yake na maisha magumu ule utakuwa mwisho. Masikini Janeth wa watu hakujua kile kinachomngoja mbele yake.

Kweli baada ya miezi mitatu Johnson siku alipojua Janeth ameingia hedhi, Johnson alifanya kila namna akawahi kurudi nyumbani na kumpikia Janeth. Wakati anapakua chakula cha Janeth alichanganya na zile dawa kisirisiri na kumpa Janeth.

Kisha siku tatu mfululizo aliomba ruhusu ya kuumwa kazini ili abaki nyumbani na Janeth. Kipindi hiki Janeth alishakuwa kaacha kazi kwenye lile duka na yuko kutafuta kazi nyingine. Hivyo muda mwingi alikuwepo tu nyumbani.

Ile ndiyo ilikuwa raha ya kuwa na mwanaume anayekujali kwa kila kitu. Angalau hivyo ndivyo Janeth alidhani, masikini hakujua mipango ya Johnson.

Basi Johnson zile siku tatu alijitahidi kuonyesha upendo sio wa kawaida kwa Janeth na alifanikiwa hata kubeba zile pedi huku akimdanganya Janeth kwamba alizichoma moto.

Johnson alifanya kila kitu kama yule mganga alivyoagiza na mpaka zile pedi zilifika kwa yule mganga.

Baada ya kukamilisha hayo yote, Johnson alianza kuona mabadiliko kwenye maisha yake. Kwanza aliongezewa mshahara bila sababu. Baada ya miezi sita tu ya kufanya lile jambo akapandishwa cheo. Kila mtu kazini mpaka akawa anashangaa huyu kijana anafanya nini kinachoonekana bora kuzidi wengi?

Ukweli ulikuwa kwamba kitendo alichokifanya Johnson, kilifanya nyota ya mvuto ya Janeth ihamie kwa Johnson na kumpelekea haya mafanikio yote. Janeth ikawa ngumu kwake kupata kazi, badala yake Johnson akampa mtaji uliotosha Janeth kufungua duka lake yeye mwenyewe la vyombo. Janeth akawa anaagiza mizigo yeye mwenyewe kutoka China.

Pamoja na kuhangaika sana na kufanya matangazo, bado Janeth hakupendwa na watu wala duka lake halikupata sana wateja kama ambavyo alikuwa anafanya kazi kwa mtu.

Johnson aliitumia nafasi hii vizuri sana, lakini akaona haitoshi anahitahi mafanikio makubwa na ya haraka zaidi. Miaka miwili baadae Johnson akarudi tena kwa yule mganga na kuomba amsaidie apate mafanikio makubwa zaidi. Maana Johnson alitamani sana kuwa hata kampuni yake mwenyewe.

Ndipo ambapo Johnson alipewa masharti mapya kwa ajili ya hii safari mpya. Johnson aliambiwa kwamba kilichobaki kufanya sasa ni kumtoa kafara Janeth, lakini si hii kafara waliyozoea watu.

Kafara ya Janeth haitakuwa ya mwili bali ni ya roho na haitazikwa roho yake peke yake.

Ilitakiwa Janeth alale na wanaume tofauti na Johnson watatu. Kitakachotokea ni kwamba kila mwanaume atakaye lala na Janeth itachukulia nyota yake ya mafanikio na kiasi cha roho yake bila yeye kujua.

Na katika wakati huu wote Johnson hakutakiwa kabisa kukutana kimwili na Janeth ili yeye awe salama. Sharti la safari hii ilikuwa gumu kidogo kwa Johnson. Hakuwahi kuweza kukataa tendo kwa Janeth mara akiona tu mwili wa Janeth na ule urembo wake.

Basi akaambiwa ili hayo yafanikiwa kuna dawa nyinigine atapewa. Dawa hii ahakikishe anaipata kwenye uume wake na nyingine kuweka mdomoni siku anakutana kimwili na Janeth. Na hiyo siku ahakikishe ni siku ambayo Janeth anaingia hedhi ili dawa ile iweze changanyika na damu ya hedhi ya Janeth.

La muhimu alilosisitiza mtaalamu ni Janeth aache kwenda kanisani kuanzia muda huo. Na vyovyote itakavyokuwa, siku ambayo Johnson atakutana kimwili na Janeth, Janeth asisogelee kabisa kanisa, kumumba Mungu wala kushika biblia.

Haya maelekezo ya kanisa yalikuwa maalumu sana kwa sababu Janeth aliendelea kujitahid sana kumuomba Mungu na kwenda kanisani kutubu maovu yake ya nyuma.

Kwa wasiwasi mwingi Johnson alipokea maelekezo mapya na dawa husika toka kwa mtaalamu na akaahidi kwenda kuyafanyia kazi.

Janeth ambaye hakuwahi bishana na Johnson vikali, siku anaambiwa aache kwenda kanisani kuanzia muda huo, alikuwa na ubishi wa hali juu. Vita ilikuwa kali sana ndani ya nyumba yao.

Pamoja na kubisha kote na kutoa sababu zote za msingi Janeth hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kukubaliana tu na yale aliyoyataka Johnson.

Binti wa watu aliacha kuendelea kwenda kanisani na hata nguvu yake ya maombi ilizidi kupungua vikali.

Kuanzia muda huo Johnson akawa mtu anayezingatia sana mzunguko wa hedhi ya Janeth. Alijifanya ni mtu aliyejaa sana upendo kwa Janeth. Hata Janeth mwenyewe akaamini kwamba Johnson anazidi kumpenda. Hata yale mawazo ya kuzuiliwa kwenda kanisani yalianza kupotea. Janeth akaanza kujikuta anarudi kwenye hali yake ya nyuma kuwa mtu asiyejali chochote.

Akawa ni mtu wa kutoka na rafiki zake kwenda viwanja vya starehe. Janeth akazidi kurudi nyuma na kuwa mwanamke anayetamani sana wanaume kila mara anapoona mwanaume anayemvutia.

Kwa muda wa miezi mitatu tu, Janeth alibadilika sana tofauti na kawaida. Ajabu ikawa ni Johnson wala hata hakumzingatia katika hizo shida, bali alizidi kumpa pesa za kwenda kutumia hizo sehemu za starehe.

Siku ilipowadia mtaalamu alimpigia simu Johnson na kumkumbusha kwamba siku wamekuwa wakiisubiri sana sasa imewadia. Imebaki kwake Johnson kukamilisha zoezi ikiwa bado anadhamilia kuwa na mafanikio zaidi.

Ingawa alikuwa na wasiwasi ila Johnson alikuwa tayari kuendelea na mpango wao. Siku hiyo ilikuwa ni majira ya saa nne asubuhi Johnson alipokumbushwa. Bila kuchelewa aliondoka kazini na kurudi nyumbani.

Siku ambazo Janeth alitegemea kuanza ingia hedhi alipenda kushinda tu nyumbani. Maana maumivu alikuwa anayapata hayakuwa ya kawaida, tofauti ilivyo kwa wanawake wengine wa umri wake.

Alipofika tu nyumbani Johnson anaonana na Janeth na kupokelewa na maswali.

Janeth: Vipi mpenzi kwema, mbona umetoka kazini?

Johnson: Nimeomba ruhusu nimewaambia nina mgonjwa anahitaji msaada wangu.

Janeth: Huyo mgonjwa nani tena?

Johnson: Hahahaha! Kweli unajifanya hujui nani anaumwa?

Janeth: Kweli mimi sifahamu honey. Niambie basi.

Johnson: Ni wewe mama angu. Unaingia period leo nimeona kama kawaida nikupe kampani.

Janeth: Aah! Baby bwana ungeendelea tu na kazi hali ya kawaida hii.

Johnson: Wala usijali. Alafu nimezungumza daktari mmoja hivi amesema kabla hujaanza period tukifanya mapenzi inaweza kusaidia kupunguza maumivu.

Janeth: Mmh! Mbona sijawahi kusikia hicho kitu? Hata hivyo nahisi tayari imeanza mbona.

Johnson: Haina shida tunaweza kujaribu.

Janeth: Mmmh hapana aisee na hii hali si sawa tusije kupata magonjwa.

Johnson: Tujaribu tukiona tu hata dalili za damu tunaacha.

Janeth: Wewe utakuwa tu na hamu zako huko hakuna lolote. Natangulia ndani mimi utanikuta.

Johnson moja kwa moja akaenda chooni na kuweka dawa kiasi mdomoni na nyingine akapaka kwenye uume wake. Akarudi ndani na kukuta Janeth tayari yuko zake kitandani kajilaza kimitego.

Janeth alikubali lakini moyoni mwake alikuwa hajakubaliana kabisa na suala hili. Johnson alifanikiwa alichokusudia na Janeth hakugundua chochote. Ila tu kweli siku hiyo aliona kuna mabadiliko hakupata maumivu kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma. Walicheka na kula pamoja siku hii wakiwa na furaha.

Walitaniana sana mpaka ilipofika usiku muda wa kulala waliendelea kuwa na furaha, lakini Janeth alianza kuweweseka na ndoto za ajabu hiyo siku. Mara anaota majini yamechukua damu yake wanakunywa. Kila akihisi kushituka toka usingizini anashindwa kufumbua macho na kuamka wala kutoa sauti.

Ghafla kwenye ndoto anaona watu wanakula nyama za watu na katika wale watu mmoja wao ni Johnson. Mchumba ambaye wanapenda sana anawezaje kuwa mmoja wa hao watu? Pale walipokaa wale watu kuna mzee mmoja aligeuka na kumuangalia Janeth. Kisha akasimama kumfuata na kumwambie, “Najua una njaa ili hii nyama haikufai binti yangu.” 

Janeth alishindwa kujizuia akauliza, “Kwani nyie ni kina nani na mbona hiyo nyama ni viungo vya watu?” Mzee akajibu kusema, “Mengine hayakuhusu, kwa sasa wewe utatuletea tu roho za watu ili majini yapate chakula chao na nyie muendelee kuwa na matajiri.” Janeth akshtuka haraka toka ndotoni huku akisema kwa sauti, “Yesu baba angu nisaidie”. Aliposhituka ndipo anatambua Johnson hayuko pale kitandani.