“Johnson” Kwa sauti kubwa ya ukali uliochanganyika na uoga Janeth alimuita mpenzi wake. Ambaye hakuwepo chumbani wala sebuleni. Mwili wote wa Janeth ukawa unatetemeka kwa baridi alilokuwa anasikia na hapo haelewi ni nini anatakiwa kufanya.
Mpenzi wake haonekani ndani ya nyumba na ni usiku atakuwa ameenda wapi.
“Au ile ndoto ilikuwa ya kweli” Kwa sauti ya chini alijiuliza Janeth akiwa amekunja mikono yake kama kujikumbatia. Akaendelea kuwaza kwamba hiyo haiwezekani ile ilikuwa ndoto tu.
Akiendelea kuwaza akaona ngoja aende chumba cha wageni kuangalia labda yupo huko. Kufungua mlango kweli anamkuta Johnson amekaa tu pale kitandani akiwa ameshika picha ya pamoja aliyopiga yeye na Janeth mwanzoni mwa uchumba wao.
Janeth: Kwa hiyo hujanisikia ninapokuita? (aliuliza kwa ukali)
Johnson: Ooh! Mpenzi pole hata sikukusikia. Vipi mbona kama umeona jini?
Janeth akashituka kusikia swali hilo maana linaendana kabisa na kile alichokuwa anaota.
Janeth: Mmh! Umejuaje?
Johnson: (kwa mshituko kuhisi ishu imejulikana) Kweli umeona jini? (Kwa haraka akasimama na kumkumbatia Janeth).
Johnson: Nini kimetokea mpenzi wangu?
Janeth: Nimeota ndoto mbaya sana na wewe ukiwemo.
Johnson: Hebu twende ndani unisimulie vizuri.
Janeth: Hapana kule siwezi tena kulala kwa leo. Tukae tu huku huku.
Basi walikaa pale wakajifunika vizuri wakiwa wamekumbatiana na Janeth akamsimulia Johnson ile ndoto yote. Johnson akamriwadha kuwa ile ni ndoto tu haina uhalisia na yeye wala hayuko hivyo. Akaongeza kumwambia labda ameota hivyo sababu yuko hedhi alikuwa anaogopa asubuhi kulala a Johnson.
Kidogo Janeth akatulia na kuona yale anayoyasema Johnson yanawezekana.kuwa ni ukweli, lakini kwanini ameota ndoto kama hii siku ya leo? Aliendelea kujiuliza Janeth.
Wakiwa bado hawajapitiwa na usingizi Janeth akaanzisha mazungumzo na Johnson.
Janeth: Kwani ulikuwa unafanya nini na ile picha?
Johnson: Nilikosa usingizi nikawa nakumbuka kipindi tumeanza mahusiano. Ndo nilikuja huku kuangalia baadhi ya vitu vyetu vya mwanzo.
Janeth: Sasa ile picha ilikuwa inakukumbusha kitu gani?
Johnson: Ile picha tulipiga mara ya kwanza kabisa tumeenda kutembea pamoja. Ulijawa na furaha sana siku ile.
Kweli hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa wamekaa siku nzima pamoja na kufanya kila kitu pamoja. Ni siku ambayo Janeth alifurahi sana.
Stori zikaendelea wakikumbushana nyakati zao za nyuma. Kitu ambacho kilifanya Johnson ajisikie vibaya sana kwa kile alichofanya. Bahati mbaya kwa hatua aliyofikia ni kwenda mbele tu hakukuwa na namna.
Hakuwa anapenda wala kufurahia kwamba Janeth atalazimika kulala na wanaume wengine, ila inabidi iwe hivyo ili aweze kufanikiwa.
Waliendelea kupiga stori mpaka muda wote wakapitiwa na usingizi.
Hayo ndiyo yalikuwa maagano ambayo Johnson aliingia ili kupata mafanikio, na sasa ndipo anazidi kukaribia zaidi kuyafikia yale aliyoyataka.
Cheo chote alicho nacho na pesa alizo nazo sasa hivi bado hazikuwa kitu kwake. Ndoto yake kubwa ni kuwa tajiri nchi nzima imjue na awe na kampuni kubwa kama walivyo kina Bakhresa. Kwahiyo kwake kazi ndo ilikuw inaanza.
Na Peter akiweza kulala na Janeth basi hii itakuwa funga kazi kwake ili aanze kuona matunda ya kazi yake.
Siku kadhaa za ukimya zilipita kati ya Janeth na Peter bila kuwasiliana kwa chochote. Ni hali ambayo ilimkera sana Johnson maana alihitaji sana jambo hili lifanyike mapema. Akaona njia bora ya yeye kuhakikisha hili suala linawezekana ni kutengeneza mazingira ya ushawishi.
Na alihitaji hili jambo litokee kabla ya likizo yake ya December ambayo ingeanza wiki mbili kabla ya sikukuu ya Christmas.
Johnson alijua fika kwamba akirudi nyumbani kabla Peter hajalala na Janeth basi yeye atashindwa kujizuia kuwa na mpenzi wake. Na akifanya hivyo anakuwa kavunja na masharti na hajui nini kitatokea baada ya hapo.
Hivyo hakuwa na namna ilibidi afanye chochote anachoweza ili hili jambo liwezekane. Basi akaanza kufanya kila namna Peter awe anachukua vitu apeleka nyumbani kwa Janeth ili kuwakutanisha.
Peter nae akawa anaenda, lakini akifika hataki kuonana na Janeth. Anaacha tu mizigo kwa mlinzi kisha yeye anaondoka. Kila mara Janeth anaambiwa na Johnson Peter ameletea vitu hapo, lakini hata siku moja yeye hakubahatika kumuona Peter.
Hali hii ilimfanya Janeth ajawe sana na wasiwasi juu ya kwanini Peter hataki kuonana na yeye? Lakini pia akawa tayari anamtamani Peter sana tu tangu siku ile. Nae akaanza kupanga njama zake ili aweze kuonana an Peter.
Basi siku nyingine alipojua Peter atakuja, akamuagiza mlinzi ili mlangoni kusiwe na mtu muda Peter anafika. Peter alipokuja kama kawaida yake aligonga geti likafunguliwa na akaingiza pikipiki yake ndani.
Alipoingia ndani ndipo anatambua aliyefungua geti si mlinzi aliyemzoea, bali ni Janeth. Peter hakuwa na ujanja tena. Akaanza kujifanya kuongea kufincha mshtuko aliokuwa nao.
Peter: Aah! Shem vipi kwema?
Janeth: Ila wewe Peter unataka kunifanya nini mwenzako?
Peter: Una maana gani shem sijakuelewa?
Janeth: Mimi kujilegeza kote siku ile kwako ukaamua kunikimbia na hutaki kuonana na mimi. Unajua kama mwanamke najisikiaje lakini?
Peter: Lakini wewe ni shemeji yangu na mimi namuheshimu sana Johnson.
Janeth: Achana kwanza na Johnson wewe ongea na mimi au hunitaki?
Peter: Sio, hivyo shem.
Janeth: Kwanza acha kuniita shem. Niite jina langu alafu twende ndani kwanza hapa nje si sawa.
Wakaongozana na mizigo yote kwenda ndani. Peter akiwa nyuma anaangalia namna mtoto anatembea huku anatingisha. Ule ni ushawishi haswa kwa mwanaume.
Janeth: Haya hebu kaa hapo tuzungumze.
Peter: Shem. Aah! Namaanisha Janeth mimi hata sio mkaaji nitaondoka si muda mrefu.
Janeth: Hebu kaa kidogo bwana.
Peter: Najua una wasiwasi kwamba nitamwambia Johnson kuhusu ile siku. Kuwa na amani hayo yameisha siwezi mwambia chochote.
Janeth: Sawa nashukuru, ila mimi nakuhitaji wewe. Nimevutiwa sana na wewe.
Peter: Hilo halitawezekana Janeth.
Janeth: Hakuna kisichowezekana hii dunia Peter.
Janeth alisema hivyo akiwa tayari anamsogelea Peter na nguo aliyokuwa amevaa tayari ameanza kuitoa.
Haraka Peter akamrukia na kumzuia asiendelee kutoa ile nguo.
Peter: Hapana Janeth hebu tulia kwanza nisikilize ujue kwanini siwezi kufanya hili jambo na wewe.
Janeth: Au mimi ni mbaya Peter hunipendi?
Peter: Hapana sio hivyo. Wewe ni mrembo sana na hakuna mwanaume hii dunia atakataa kupata hata dakika moja na wewe.
Janeth: Sasa kwanini wewe hunitaki au wewe si mwanaume?
Peter: (Akajbu akicheka). Hapana, sio hivyo. Mimi ni mwanaume vizuri kabisa ila nina tatizo moja tu.
Janeth: Tatizo gani hilo.
Peter: Janeth mimi ni muathirika wa virusi vya UKIMWI. Na nisingependa kwa namna yoyote ile upate ugonjwa huu.
Janeth: Muongo wewe unasema tu hivyo ili nisilale na wewe.
Peter: Ni ukweli Janeth. Nimeishi na huu ugonjwa kwa miaka 15 sasa. Niliupata katika ajali moja hivi ya basi.
Janeth: Mungu wangu pole Peter (Alisema akiendelea kuvaa vizuri nguo yake na kusogea pembeni)
Peter: Asante, Siku ile nilikaa siti moja na mtu mwenye huu ugonjwa. Bahati mbaya wote tuliumia na damu zetu zilichanganyika.
Janeth: Mmh! Una roho nzuri sana Peter angekuwa mwanaume mwingine hata asingeniambia kitu kama hicho.
Peter: Wala usijali, sasa mimi naomba nikuache na usimwambie hata Johnson kuhusu hili.
Janeth: Sawa usijali siwezi mwambia mtu.
Basi wakaagana vizuri na Peter akaenda zake. Tangu siku hiyo waliendelea kuwasiliana vizuri bila shida na Janeth hakuendelea tena kumtaka Peter. Pamoja na hilo bado Janeth aliendelea kuwa kama mtu mwenye pepo la ngono. Kila mara alizidi kujisikia kuwa na hamu isiyo ya kawaida.
Alitamani karibu kila mwanaume aliyekuwa na mvuto hata kidogo machoni kwake. Hali ilizidi kuwa mbaya mpaka yeye mwenyewe akabaki kujishangaa ni nini hiki kinamjia. Katika hali isiyo ya kawaida akagundua kwamba pamoja na hamu zote hizo, hakuwa anamtamani mpenzi wake Johnson.
Johnson akiwa anajipa moyo kwamba huenda Peter na Janeth tayari wamekamilisha tendo alianza mipango ya yeye na Janeth kwenda likizo visiwani zanzibar pindi atakaporudi.
Aliashataka kuanza kuandaa safari yote mpaka hoteli watakayofikia, lakini mipango yake ilikatishwa na mtaalamu wake siku alipo ambiwa kwamba Peter hakufanikiwa kulala na Janeth.
Taarifa hii ilimfikia Johnson siku mbili kabla ya likizo yake kuanza na tayari alishakuwa amemtaarifu Janeth juu ya likizo yao. Sasa wakienda hii likizo ni wazi yeye atalala na Janeth kabla mpango wake haujakamilika.
Johnson alijawa sana na hasira na kukata tamaa akajua kabisa kwamba huu ni mwisho wa mafanikio aliyo nayo na hata anayoyategemea. Dawa aliyotumia siku ile inafanya kazi yake kumpa Janeth hamu kila mara, lakini bado Janeth hakuweza kulala na Peter.
Siku hii Johnson hata hakuangaika kumpigia simu Janeth asubuhi wala mchana. Walikuja kuongea jioni kabisa muda Janeth amepiga kumjulisha kuhusu safari nyingine ya kwenda Moshi.
Mchana wa siku hiyo shangazi yake Janeth almpigia simu na kumfikishia maagizo kutoka kwa baba yake Janeth. Kwa miaka miwili mfululizo Janeth hakuwahi kwenda kwao Moshi kusalimia. Safari kaambiwa ahakikishe shangazi yake anapoenda Moshi na familia yake nae aende. Kama si hivyo basi yule si baba yake kuanzia muda huo. Hivyo ilibidi kwa namna yoyote ile afike Moshi.
Masikini Janeth wa watu alitumia nguvu nyingi sana kujieleza kwa mpenzi wake na kuomba msamaha kwa kuharibu mipango yao. Kitu hakujua ni kwamba taarifa hii ilikuwa njema sana kwa Johnson. Maana ilimaanisha Janeth hatokuwa pamoja nae kwa muda wote wa likizo.
Johnson: Usijali mama angu wazazi ni muhimu sana. Nenda ukawasalimu na uwasikilize wana nini ya kusema.
Janeth: Nashukuru kwa kuelewa mpenzi. Nitajitahidi niondoke kule mapema baada ya tu ya Christmas kupita.
Johnson: Usijali mimi nitaangalia namna niongeze likizo ili tuwe wote, kwa sasa wewe zingatia kuwa mtoto mwema.
Janeth: Sawa baba angu. Basi Kesho asubuhi mapema ndo safari inaanza.
Johnson: Ooh kumbe mapema hivyo?
Janeth: Ndiyo, maana tunaenda na kina mjomba na Shangazi.
Johnson: Mnaenda na usafiri gani.
Janeth: Sijajua, ila kwa ninavyomjua mjomba lazima atasema Shangazi aende na gari yake na yeye na yake anapenda sana kujionyesha.
Johnson: Hahaha si kama wewe tu kuwatambia wenzako. Anyway sawa haina shida muwe na safari njema nipigie asubuhi kabla hamjatoka.
Waliagana vizuri na kila mtu akaendelea na ratiba zake.
Asubuhi kweli Janeth alikuja kuchukuliwa na mjomba wake, na kama alivyotabiri shangazi yake alikuwa na gari yake Range rover Velar 2023 na mjomba alikuwa na yake Land Cruiser LC 300.
Shangazi alikuwa na mwanae wa kwanza wa kiume na dada wa kazi. Mjomba alikuwa na binti yao wa pili tu. Basi Janeth akapanda gari ya mjomba na safari ya kwenda Moshi ikaanza.
Safari ambayo aidha itaokoa mpango wa Johnson au ndiyo itakuwa safari inayouzika kabisa mpango wake wote.
Safari hii ilitegemewa ndiyo ya mwisho kwa Janeth kwenda kulala na mwanaume mwingine. Safari nzima mjomba alipiga stori na Janeth. Mjomba alimkubali sana Janeth maana ni binti aliyejitambua na alikuwa mpambanaji sana.
Bahati mbaya Janeth si siku zote alipenda kuwa karibu na mjomba wake maana mara nyingi alimsikia shangazi yake akisema mjomba wake ni mtu penda penda sana. Ila tu raha yake ni mtu anayeijali familia yake.
Hii kwa Janeth bila yeye kujua itakuwa ni safari yenye mitego sana na huenda ndiyo kifo chake cha kiroho. Safari ambayo inaenda kuwakutanisha watu wengi pamoja na yenye ushawishi mwingi ukijumlisha unywaji wa pombe.
Katika hali yake ya kutamani sana wanaume, Je Janeth atakuwa salama? Hii hali ambayo kwake anaona ni mahitaji tu ya mwili. Ataweza kuvumilia au atakubali madhaifu aliyo nayo?