HABARIDUKA - Tanzanian Digital Marketplace
Back to Story
Nyota Ya Mrembo Aliyezikwa Hai - Chapter 5: Bei ya Mafanikio ya Johnson

Nyota Ya Mrembo Aliyezikwa Hai - Chapter 5: Bei ya Mafanikio ya Johnson

Mjomba: Janeth, biashara yako inaendeleaje sasa hivi?

Mjomba aliuliza swali ambalo halikupewa majibu. Janeth alionekana kuwa na mawazo mengi akili yake haikuwa pale kabisa. Tangu wameanza safari mara kwa mara mjomba ilibidi amshtue Janeth ili waweze kuzungumza. Muda wote akii ya Janeth ilijawa na wasiwasi na mawazo mengi.

Janeth alikuwa na hofu, lakini hakujua hata ni nini anaogopa. Muda mwingine alijikuta akikumbuka ndoto za ajabu alizokuwa akiota hivi karibuni, lakini kitu kilichukua sana akili yake ni maneno aliyoambiwa na shangazi yake kwamba asipokwenda safari hii kwao amsahau baba yake mzazi.

Wazazi wa Janeth walikuwa ni watu ambao walimcha sana Mungu miaka yao yote. Imani yao haikuwa tetereka na wao waliamini mafanikio ni kuwa na familia yenye furaha.

Mara kwa mara walimshinikiza binti yao kushika sana imani yake na kuomba Mungu mara kwa mara. Shida sasa binti mwenyewe ndo huyu Janeth. Mtoto wa mjini anayependa maisha ya raha.

Mjomba aliendelea kujaribu kufanya mazungumzo na Janeth ili kumtoa mawazo, lakini haikuonekana kuzaa matunda yoyote. Mpaka sasa ikabidi mjomba ahoji tu moja kwa moja kwa kuuliza, “Janeth binti yangu kwani shida ni nini?” badala ya kujibu Janeth aliangua kilio. Machozi yalimbubujika mengi mpaka mjomba alipata wasiwasi.Ikabidi amuache kwanza bila kusema kitu mpaka atakapoacha kulia yeye mwenyewe.

Safari yao iliendelea kwa muda kidogo huku Janeth akiendelea kulia kimya kimya mpaka pale walipofika sehemu ya kula, ambapo mjomba alimshawishi Janeth ashuke kwenye gari lakini aligoma.

Moja kwa moja binti wa mjomba alishuka mbio na kukimbia kwa mama yake.

Binti: Mama! mama! Njoo uone dada Janeth analia huku.

Shangazi: Analia? (alihoji kwa mshangao) Analia kisa nini?

Binti: Hata sijui labda baba amempiga.

Alijibu yule binti bila wasiwasi. Alikuwa ni mtoto mdogo na hakuelewa mambo yanavyoenda. Muda wote wa safari yeye alikuwa amelala na ameamka muda huo walipofika sehemu ya kula.

Moja kwa moja shangazi akaelekea kwenye gari ya mme wake mbele. Alipofika tu kaanza kuhoji.

Shangazi: Mme wangu vipi tena kuna shida gani?

Mjomba akamvuta shangazi pembeni kwanza ili wazungumze.

Mjomba: Sijajua shida nini, ila muda wote wa safari alionekana kuwa na mawazo. Ameanza kulia mara tu nilipomuuliza ana shida gani.

Shangazi: Au wewe umemfokea mtoto?

Mjomba: Sasa mke wangu mimi nitaanza tu kumfokea mtu mzima hivyo?

Shangazi: Ninavyokujua mme wangu hushindwi wewe.

Mjomba: Sitaki kuharibu siku. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Huenda ni mambo yenu ya kike. Nenda zungumza nae wacha mimi niende na watoto kula.

Wakakubaliana na mjomba akachukua watoto kwenda kula. Shangazi akarudi kuzungumza na Janeth kwenye gari. Alipofika tu kwenye gari na kuita jina la Janeth. Janeth aligeuka haraka na kumkumbatia shangazi yake kwa nguvu mno.

Shangazi alielewa mambo ya watoto wa kike vizuri sana na hata hakuangaika kusema kitu. Kwa zaidi ya dakika tani walikaa pale wakiwa wamekumbatiana bila kusema chochote mpaka Janeth akamaliza kulia na kuanza kuongea.

Janeth: Asante, shangazi hii safari nadhani itakuwa msaada mkubwa sana kwangu.

Shangazi: Usijali mwanangu. Kama tu uko sawa hilo ndilo la msingi. Si lazima kuongelea shida iliyopo kama hutaki.

Janeth: Ni vile tu sielewi maisha yangu shangazi. Napata kila kitu ninachohitaji, lakini bado nafsi yangu haina amani na naona kuna kitu nakosa.

Shangazi: Muombe sana Mungu utakuwa sawa. Na kama ukiona siku na mwenzako kuna shida hamuelewani muda wowote uje nyumbani. Mimi na mjomba wako tutakupokea.

Janeth: Sawa shangazi lakini nisingependa kuwasumbua.

Shangazi: Janeth, mwanangu tangu umefika Dar Es Salaam kusoma na kumaliza masomo hukuwahi kukubali msaada wangu kwa lolote. Najisikia vibaya kuona unateseka na mimi nipo hapo hapo.

Janeth: Hapana shangazi sio nateseka, nilitaka nijifunze maisha na niwe imara kama wewe.

Shangazi: Sawa sasa umejifunza vya kutosha. Wakati ujao uwe unakuja kujiunga nasi walau uwe karibu na familia yako.

Janeth: Sawa shangazi.

Wakaendelea kuzungumza kwa dakika chache tena kisha wakashuka kuelekea kula pia. Walikula pale wakifurahi vizuri kama familia na hakuna mtu mwingine alijua nini kimezungumzwa kule kwenye gari.

Kwa muda mfupi kutoka kwenye chakula mpaka wakaendelea na safari hadi kufika nyumbani Janeth akawa ni mtu mwenye furaha na mcheshi mpaka mjomba akabaki kushangaa imekuwaje tena. Ila akajisemea tu kwamba watoto wa kike ndivyo walivyo. Dakika moja mnaelewa dakika nyingine hawaeleweki.

Kule moshi walipokelewa vizuri kwa shamra shamra nyingi sana. Familia za kina mjomba na shangazi zilikuwa kijiji kimoja nyumba za jirani tu. Mjomba na Shangazi walianza mahusiano yao wakiwa wadogo sana tangu wapo hapo kujijini wakiwa wanasoma.

Mapenzi yao yalidumu mpaka wamefunga ndoa, wamebarikiwa watoto wawili na sasa wanaishi nyumba yao na wana biashara zao wenyewe. Haya ndiyo maisha Janeth aliyatamani sana, lakini mpaka sasa bado hajabahatika kuwa nayo.

Japo kuwa Johnson aliweza kumfanyia kila kitu ila bado aliona haitoshi. Mahusiano ya mjomba na shangazi yake ndiyo maisha aliyatamani sana. Na ndiyo ilikuwa sababu ya yeye hata kuanza mahusiano na yule kijana wa chuo anayeitwa Brian.

Walipopokelewa tu dakika chache baadae Janeth alivutwa pembeni na wazazi wake. Walijawa na furaha sana kumuona mwanao ambaye kwa muda mrefu hawakumuona na sasa amekuwa binti mtu mzima mwenye maisha yake mazuri huko mjini.

Ila wamemlazimisha sana kuja safari hii kwa sababu ya maono ya mama yake.

Walienda kukaa chini ya mti pembeni kidogo ya nyumba. Mahali ambapo tangu utoto wa Janeth baba yake alipenda sana kukaa hapo jioni akiwa anawapa wosia watoto wake kuhusu maisha na kuwapa stori mbalimbali za enzi zake.

Baba: Janeth mwanangu!

Janeth: Abee baba.

Baba: Sisi tumefurahi sana kukuona uko mzima, una afya njema, lakini sura yako inakosa nuru. Inaonekana furaha ni jambo geni kwako. Sisi hatutauliza shida nini ila mama yako ana jambo anataka kukwambia.

Janeth alihisi labda ameandaliwa mume wa kumuoa huku kwao. Maana kwa muda mrefu wazazi wamekuwa wakimuuliza huyu bwana ake Johnson atarasimisha lini ile wafunge ndo iliyobarikiwa na Mungu.

Lakini hii haikuwa jambo ambalo wazazi wake walitaka kumwambia. Mama aliponyanyua tu kinywa chake kuanza zungumza michozi ilianza kumwagika. Kitendo ambacho kilimfanya Janeth pia aanze kulia.

Baba: Mama Janeth hebu acheni kulia. Mnataka watu watuone huku.

Baada ya baba kuwasihi hivyo kulikuwa na kimya kwa dakika mbili ndipo mama akaanza kuongea. Mama akaanza kumwambia Janeth kuhusu maono aliyoonyeshwa na Mungu wakati anasali.

Mama akamsimulia Janeth kwamba ameonyeshwa na Mungu kwamba kuna mtu wa karibu sana na Janeth hana nia njema na yeye. Mtu huyu anaonekana kuwa na upendo mkubwa kwa Janeth na Janeth pia anampenda sana. Lakini huu upendo wao unazidi kupungua siku hadi siku kulingana na namna ya maisha yao.

Kinachofanya upendo wao upungue ni mambo ambayo huyu mtu anayafanya juu ya Janeth. Ni kwamba huyu mtu ana nia ovu juu ya binti yao Janeth. Janeth asipokuwa makini maisha yake yatakuwa magumu mno.

Baada ya kusikia haya yote Janeth alibaki kimya akiwatazama wazazi wake. Alisita kusema kile alichokiwaza kwamba huenda huo ni uoga wao tu kwa sababu yeye yuko mbali. Lakini mara nyingi kila utabiri wa mama yake ulitimia. Hiyo ndiyo kitu ilimuogopesha sana Janeth.

Walimaliza mazungumzo yao kwa maombi na kila mmoja akaendelea na mambo mengine. Wakarudi kujumuika na ndugu wengine palae nyumbani kwao.

Familia zote mbili ziliendelea kuisubiri Christmas ifike muda wote wakiwa watu wenye furaha na shamra shamra nyingi. Siku ya mkesha wa sikukuu ya Christmas watu wote walikuwa pamoja wakifurahi.

Mkesha ukiendelea Janeth alitoka na kwenda pembeni kidogo akawa amekaa chini kimya akampigia simu mpenzi wake Johnson. Mara tatu alipiga simu ikaita bila kupokelewa.

Kwa mara ya kwanza Johnson hakupokea simu yake na hakusema kama atakuwa na kazi. Alipata wasiwasi na akaendelea kukaa pale akiwaza. Akiwa ameketi pale peke yake, mjomba nae akawa amechoka kwenye watu wengi asogee pembeni pia akiwa anaongea kwenye simu.

Alipomaliza kuzungumza na ile simu mjomba anageuka na kumuona Janeth.

Mjomba: Janeth vipi mbona peke yako huku?

Janeth: Salama mjomba, nilitaka kuongea na mtu sasa simu yake haipatikani.

Mjomba: Ooh pole labda atakuwa kwenye kelele tu hajaisikia simu.

Janeth: Mmmh! Si mtu anayependa kelele wala kujichanganya na watu na haijawahi tokea hivi.

Mjomba: Bila shaka ni mpenzi wako?

Janeth: Ndiyo mjomba.

Mjomba: Mapenzi machanga hayo. Usijari hakutakuwa na shida. Na hata kukiwa na shida wewe ni msichana mrembo sana mpwa wangu. Utapata wengine wengi na utasumbua wengi mjini.

Janeth: Hahahahaha mjomba bwana. Huwa hupendi kabisa kuona mtu hana furaha. Asante kwa kunitia moyo.

Mjomba: Aya nyanyuka hapo turudi kule kwa wengine.

Basi wakatoka pale na kurudi kule walipo watu wengine. Wakaendelea na stori mpaka usiku wa manane. Lakini muda wote mjomba alizidi kumtazama sana Janeth kwa jicho la maswali mengi.

Ni kama mtu aliyemuonea huruma, lakini pia kama ana upendo nae wa kipekee. Ulipofika muda wa kwenda kupumzika watu waligana na kila mtu akaondoka zake. Mjomba alimuaga Janeth kwa namna ya kipekee sana. Alimshika mkono katika namna ya ushawishi na kumwambia, “Uwe na usiku mwema mrembo”.

Janeth alishtuka kidogo. Ndiyo ni kawaida ya mjomba kuwatania mabinti kwenye familia yao kwamba ni warembo, lakini hii namna amemshika mkono kuna kitu Janeth hakuelewa.

Lakini pia ni kitu ambacho kilimfurahisha na kumpandisha nyege kwa hali ya juu. Kitendo kile cha mjomba kilimrudisha Janeth kwenye ile hali ya kutamani sana kulala na mwanume. Alikaa usiku mzima akiwaza namna ule mkono wa mjomba umepita kwenye mkono wake na akazidi hata kumtamani mjomba wake.

Alishindwa hata kulala usiku mzima. Alikuja kushtuka asubuhi anaambiwa aamke ajiandae waelekee kanisani kwa ijali ya ibada. Wakiwa kanisani akili yote ya Janeth ilibaki kumfikiria mjomba na macho yake yalizidi kumtazama kwa matamanio mpaka mama yake Janeth akashtuka na kumgusa kwa kibao mkononi Janeth na kumwambia, “Wewe hebu kuwa na aibu huko.”

Mama yake alimuona na akaona hali aliyo nayo mwanae na alijisikia vibaya mno kuona mwanae anamtazama mjomba wake kwa jicho la namna ile. Baada ya kitendo kile Janeth alijua fika hii siku haitaisha salama kwake.

Mama yake si mtu wa kuacha jambo lipite kimya kimya ni lazima angemsema na kumhubiria kwamba hilo ni pepo na maombi juu.

Kweli baada ya ibada kuisha na baadae kupata chakula cha mchana mama alimuita Janeth pembeni na kuanza kumpa mahubiri. Janeth alionyesha kukereka na maongezi yale, lakini hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kumsikiliza tu amalize.

Baada ya kumaliza mahubiri mama alimshika Janeth mikono na kwa pamoja walifanya maombi. Katikati ya maombi mama alimuachia mikono Janeth kama kuitupa vile na akawa amejawa na uoga. Janeth nae alikatisha maombi na kuanza kumshangaa mama yake.

Janeth: Mama vipi?

Mama: Mwanangu naona giza kubwa limekaa juu yako. Huko Dar Es Salaam unafanya nini?

Janeth: Biashara tu mama hakuna kingine. Giza kwa maana gani?

Mama: Huyu mchumba uliye nae ambaye hataki hata kuja tumfahamu anafanya kazi gani na ni mtu wa wapi?

Janeth: Mmmh! Mama kwamba unataka kusema Johnson anafanya mambo ya ajabu?

Mama: Hebu nijibu kwanza nilichokuuliza.

Janeth: (kwa uoga anajibu) Ni Boss wa kampuni moja hivi ya madini na ni mtu wa huko Lindi.

Mama: Eeh! Mungu wangu mfunike mwanangu na ulinzi wako.

Janeth: Mama mbona unanitisha?

Mama: Kuwa makini sana mwanangu, huyu kijana si mtu mzuri kwako na ikiwezekana uachane nae mara moja.

Janeth: Kwani amefanya nini?

Mama: Bado sijaonyeshwa nini anafanya, lakini naonyeshwa tu kwamba si mtu sahihi kwako.

Kwa hasira Janeth alisimama na kuondoka mahali pale akiona kama Mama yake ameanza yale mambo ya wazazi kumchagulia mtu wa kuwa naye. Janeth hakutaka kabisa kuamini kwamba Johnson anaweza kuwa mtu wa namna hiyo. Aliamini hivyo kwa sababu Janeth alijiona yeye ndiye mkosaji kwa kumsaliti Johnson zaidi ya mara moja.

Kwake aliona kwamba tangu wamekutana Johnson hajafanya jambo baya zaidi tu ya kumpa maisha bora na kumsaidia katika mambo mengine mengi. Moja kwa moja Janeth alijikuta anatoa simu yake na kumpigia Johnson. Alipopokea Janeth akamwambia kila kitu alichosema mama. Janeth alisahau kabisa kwamba usiku wa jana yake Johnson hakupokea simu na wala hakuhangaika kumrudia baada ya kuacha hizo missed calls.

Kama kawaida ya Janeth alijitenga na watu wakati anaongea na simu, na akabaki hapo akilia wakati wote baada ya kumaliza kuongea na Johnson. Alikaa pale muda mrefu na hakuna mtu alijua kwamba Janeth hayuko pale walipo.

Mjomba ndiye aligundua kwamba Janeth hayupo kwenye ule mkusanyiko pale ndani. Ikabidi atoke nje kwenda kumtafuta Janeth. Alihisi kwamba atamkuta nyuma ya nyumba ambako alimkuta jana na ndiko aliko mkuta.

Alipofika pale haraka Janeth aliacha kulia na akafuta michozi ili mjomba asione.

Mjomba: Unajua ukitaka machozi yasionekana aidha uwe na furaha kweli au ukae ndani ya maji ya bahari. (alisema kwa utani huku akicheka)

Maneno haya ya mjomba yalifanya Janeth pia acheke kwa furaha.

Mjomba: Sipendi kukuona uko hivyo. Hebu twende kwanza tukazurule huko ukae sawa.

Janeth: Sawa mjomba ila tunaenda wapi kwenye huku?

Mjomba: Umesahau kwamba mimi nimezaliwa huku. Kizazi chenu hamkuwa kama sisi. Sisi tumetembea sana huku.

Basi wakaongozana polepole wakipiga stori za mjini za biashara na maisha tu ya kawaida. Wakiendelea kutembea Janeth alifurahi sana kuona namna ambavyo mjomba anamjali na kumfanya awe na furaha. Janeth alijikuta anazidi kumpenda mjomba wake na kuzidi kumtamani na kumuonea wivu shangazi yake.

Mjomba ni kati ya wanaume wachache ambao walijua mwanamke anataka nini na anataka kusikia nini. Na hakika alimpatia sana Janeth.

Waliendelea kutembea kwa muda kidogo wakivipita vichaka vingi mpaka wakafika mahari moja pako kimya. Kelele pekee zilisikika ni zile za ndege na maji yaliyotiririka kwenye chemchem na mifereji midogo midogo kule porini.

Mazingira ya pale yalikuwa mazuri sana yaliyofanya mtu ajisikia salama na kusahau yale anayotapitia. Walipofika walienda kukaa juu ya jiwe moja na mjomba akakaa kimya bila kusema kitu.

Janeth pia alikaa kimya wakiwa pale. Ilikuwa ni wakati wa kila mmoja wao kukaa kimya na kutafakiri kivyake. Ni moja ya ule wakati ambao mnaweza kuwa pamoja kimwili, lakini kiakili kila mmoja yuko ulimwengu wa peke yake.

Wakiwa pale kimya Janeth aliomba kumkumbatia mjomba maana alihitaji sana kumkumbatia mtu ili ajisikie vizuri. Bila shaka lolote mjomba alikubali na Janeth akasogea na kumkumbatia mjomba, lakini hakuna kingine kilizungumzwa.

Mawazo yao yakiwa mbali, kwa mbali alisikika mtu mtu anakuja kama ana nyata asiwashtue. Muda wote wao hawakujua kwamba kuna mtu anakuja. Huyu alikuwa ni shangazi. Akiwa kule nyumbani alimuona mjomba anapotoka na pia hakumuona Janeth eneo lile.

Alijua namna mme wake hapendi kuona mtu anajisikia vibaya au kukosa amani. Tangu ile siku ya safari mjomba alipoona Janeth amelia vile amekuwa ni mtu anayemzingatia sana Janeth na kutaka kufanya namna yoyote awe sawa.

Hivyo shangazi alijua tu kwamba mjomba lazima ameenda kumtafuta Janeth. Shangazi alipofika pale na kuwaona akasema, “Nilijua utakuwa umemleta huku.”

Janeth ambaye akili yake ilianza kumuwaza mjomba katika mawazo yasiyo sawa. Alimuwaza mjomba anautamu gani kitandani. Janeth aliwaza sana anaweza kumshawishi vipi mjomba mpaka hata akapata penzi lake. Akili ya Janeth haikuwa pale kabisa na hata hakutegemea shangazi angekuja mahali pale.

Janeth alishtuka vibaya sana kama mtu kaona nyoka chumbani kwake. Alipogeuka na kuona ni sura ya shangazi yake mapigo yake ya moyo yalimuenda mbio mno na akajawa wasiwasi mwingi. Ni kama aliona shangazi yake anaona na kuyasikia mawazo yake.