Acha Kuwa Mtumiaji wa Internet Tu... Anza Kuimiliki. Kuna Watu Wanalipwa Kila Siku Kwa Taarifa Unazosoma Bure Google.
Kila siku unaingia Google kutafuta majibu.
Lakini umewahi kujiuliza...
Nani anaandika hayo majibu unayo yasoma?
Jibu ni rahisi.
Ni watu wa kawaida kama mimi na wewe.
Tofauti ni kwamba wao waliamua kujenga website, wewe ukaamua kuendelea kuwa msomaji.
Hiyo ndiyo tofauti.
Kama una ujuzi au unapenda mada fulani, unaweza kuanzisha Blog au Website inayozungumzia eneo moja tu (niche).
Kwa mfano unaweza kuandika kuhusu:
• Ajira Tanzania
• Scholarship na fursa za masomo
• Teknolojia na AI
• Habari za mpira
• Fedha binafsi na uwekezaji
• Utalii na maeneo ya kutembelea
Usijaribu kuandika kila kitu.
Chagua eneo moja, halafu litawale.
Kadri unavyoandika content nyingi zenye thamani, ndivyo watu wengi wanavyoanza kukutafuta kupitia Google.
Na watu wakianza kuja kwenye website yako...
Ndipo fedha zinaanza kuingia.
Unaweza kupata kipato kupitia:
- Google AdSense kwa kuweka matangazo kwenye website yako.
- Affiliate Marketing kwa kupendekeza bidhaa au huduma na kupata commission kila unapouza.
- Sponsored Posts ambapo kampuni zinakulipa uandike au utangaze huduma zao kwa sababu tayari una audience.
Kosa ambalo watu wengi wanafanya ni kutaka matokeo ndani ya wiki mbili.
Website siyo betting.
Website ni kujenga mali ya kidijitali.
Unaandika article leo...
Inaweza kuendelea kukuletea wasomaji na kipato hata baada ya miaka mitatu au mitano bila kuiandika tena.
Hicho ndicho kinaitwa asset.
Watu wengi wanatumia internet kutengeneza engagement kwenye kurasa ambazo si zao.
Wengine wanatumia internet kujenga website ambayo itakuwa mali yao milele.
Swali ni moja tu...
Je! Baada ya miaka mitatu, unataka uwe unamiliki audience yako... au bado uwe unaisaidia Google kuwatajirisha wengine?
P.S. Kama umesoma mpaka hapa, basi tayari umeelewa kwamba internet inaweza kuwa chanzo cha kipato, si sehemu ya kutumia muda na bando pekee.
Kama unataka kujifunza jinsi ya kupata pesa kupitia Affiliate Marketing, nina eBook yangu ya "Affiliate Marketing" ambayo inakufundisha hatua kwa hatua namna ya kuanza, hata kama wewe ni beginner.
Get your copy: Affiliate Marketing for Beginners
Usiache internet iwe sehemu ya kutumia pesa tu. Ifanye iwe sehemu ya kuzalisha pesa.