Leo nimesoma stori ya kijana mmoja wa miaka 20 aitwaye Michael.
Alitengeneza app inayoitwa Go Tall.
Kazi yake ni moja tu...
Inakadiria urefu ambao mtu anaweza kufikia.
Ndivyo ilivyo. Hakuna kingine.
Niliposikia wazo hilo nilicheka.
Nikajiuliza, "Hii kweli inaweza kumuingizia pesa?"
Lakini nilipofuatilia zaidi nikagundua kitu kilichonishtua zaidi...
App hiyo inaingiza zaidi ya $100,000 kila mwezi.
Swali likawa moja tu...
Inawezekanaje?
Jibu nililopata lilinifanya nibadili namna ninavyo yaona mawazo ya biashara.
Hakuna wazo la kijinga.
Ndiyo, yapo mawazo yenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko mengine.
Lakini tusicho kijua ni kwamba...
Karibu kila wazo linaweza kufanikiwa kama ukijua kulitangaza na kulifikisha kwa watu sahihi.
Hapo ndipo watu wengi hushindwa.
Michael hakubuni hata hilo wazo mwenyewe.
Aliliona kwenye comment ya video ya TikTok.
Kisha akafanya mambo matatu:
• Akatengeneza video karibu 10 za TikTok kila siku kwa mwezi mzima.
• Akawafundisha creators wengine kutumia mtindo huo.
• Akaanza kuweka matangazo ili kufikia watu wengi zaidi.
Ndiyo maana app ambayo wengi wangeiita "wazo la kipuuzi" ikawa biashara ya mamilioni ya shilingi kila mwezi.
Kilicho nigusa zaidi ni ushauri wake alio utoa kwa watu wengine.
...Acha kuongozwa na ego.
Fungua kamera. Tengeneza content.
Ongea kuhusu wazo lako hata kama watu wanakuambia haliwezekani.
Kwa sababu watu wengi hawaogopi kushindwa.
Wanaogopa kuonekana wajinga.
Na huo ndio unaweza kuwa ushindani wako mkubwa.
Kama una wazo...
Hata kama unaona ni la kawaida sana au watu wanakucheka...
Anza kulijenga. Anza kulionyesha hadharani.
Huenda kesho likawa chanzo cha kipato ambacho leo hakuna anaye kiamini.