Content Creators wengi wa Afrika ni Masikini na hata si jambo la kushangaza. Wengi wanaishi maisha ya mtandaoni ya kuonyesha wako vizuri, ila uhalisia wa maisha yao ni tofauti kabisa.

Mpaka unapo maliza kusoma hili andiko, creator wa Tanzania mwenye followers 500K anaweza kuwa amepata dili la brand ambalo watampa pesa kidogo na T-Shirt kadhaa.

Mwaka 2026 tunaona soko la content creators linavyokuwa. Mpaka serikali imetenga fungu kwa ajili yao.

  • Tamaduni tunayo.
  • Audience ipo.
  • Engaging content tunazo.

Lakini ukisoma ripoti za hili soko hivi karibuni zinasema “content creators 6 kati ya 10 Africa wanapata chini ya $100 kutokana na content zao.” Inashangaza kuona creator mwenye maelfu ya followers na views anahangaika na kulipa kodi ya chumba cha 100,000.Jibu la hii yote ipo katika mfumo. Creators wachache walioujua na kuushinda mfumo wameweza kujenga nakumiliki magari mazuri.

Na siri sio katika brand deals, bali ni katika kuuza kwa mteja moja kwa moja. Wamefanya ujenzi wa kidijitali kuhakikisha audience anapanga kwenye content zake. Nataka ujue ni kwanini model ya zamani ya kutegemea brand deals hailipi sana sasa hivi.

VIEWS ZINAWADANGANYA. Hizo ndizo Platforms zinataka muwe nazo ila sio mtengeneze pesa.

Kama unasubiri TikTok au Youtube ikupe utajiri Africa unachelewa sana. Ni unacheza mchezo wa pata potea. Sio kwamba huwezi tajirika kwa Youtube TZ, inawezekana ila kuna vitu lazima ufanye tofauti.

Kwanini nasema haiwezekani kutajirika kwa Youtube na TikTok Tanzania?

  1. Geo-Restricted Funds (pesa zinazotegemea ulipo). TikTok, Youtube na wengine wote pesa zao wamefunga ndani ya mabara mawili - Amerika ya Kaskazini na ULAYA. Ukiwa jiji kama New York views million 1 kutoka New York inakupa mshahara wa engineer Tanzania kwa mwezi, ila views 1M kutoka Tanzania zinakupa comments za “unajua sana bro” au “hii kali mzee”.
  2. Low CPM (hela inayolipwa kutokana na watu 1000 wanaoangalia content yako). Hata kwa platform zinazolipa creators Africa zinalipa pesa ndogo kwa views 1000. Yani views 1000 kutoka US zinaweza kukupa $100 ila Views 1000 kutoka TZ zinakupa $1 mpaka $3.
  3. Unyonyaji kutoka brands zenyewe. Creators wa TZ wanachukuliwa kuwa na njaa sana. Brands zinajua hilo na wanajua kwamba una njaa sana ya kupata hata hela ya kula tu. Kwahiyo wanatoa pesa kidogo ili ufanye kazi kubwa. Yani wewe ni media agency inayotembea lakini dili unazopewa haziendani kabisa na thamani yako.

Ni kwamba haumiliki audience yako, badala yake huwa unawakodisha kwa muda mfupi kwa brand mbali mbali ili upate hela ya chakula. Ila usichojua ni kwamba hiyo Algorithm ya mtandao wa kijamii unayotemea inaweza kukutema kesho tu.

2026 inabidi ubalike. ACHA kuwa INFLUENCER, badilika uwe Muuzaji wa Kidijitali.

Creators wote waliopiga hatua hawauzi audience yao kwa brands. Badala yake wanauza maarifa na ujuzi wao kwa audience wao. Hii ina maana ya kwamba unachukua kile unachokijua na unachokiweza unakiweka katika Hadithi, eBook au Kozi. Fikiria hivi

  • Mchekeshaji anayeuza comedy exclusive ambazo uncensored kwenye platform tofauti na hizi za bure.
  • Tech reviewer anayeuza blog posts zake na guides mbalimbali za tech.
  • Fitness Trainer anayeuza video zake za training na pdf za workouts za siku 30 kabla hujaenda dinner date na mrembo wako.
  • Event Organizer anayeuza tiketi kidijitali badala ya kunangaika na hard copy.

Unapouza bidhaa za kidijitali faida yako inakaribia kufika 100%. Ni kwa sababu unatengeneza bidhaa mara moja ila unauza milele. Niliacha andika magazine mwaka 2021 ila mpaka leo bado nazisambaza kwa watu.

Creators wa Tanzania wengi swali lao lilikuwa “sasa nafanyaje niwe na platform ya kuuza na napokeaje malipo?

Kila wakiangalia mifumo ya malipo ya Paypal na Stripe ni kizungumkuti. Yani ni kitendo cha kugusa tu unakuwa banned na hela zinaenda. Na kuna muda unapoteza sana wateja sababu Watanzania hawatumii sana credit cards kwenye kufanya malipo. 

Hiyo sasa ndo sababu HabariDuka kwa haraka inakuwa platform kwa ajili ya creators wa Tanzania na Afrika mashariki kuweza kuuza na kusambaza kazi zao za kidijitali. 

Habariduka sio link tu ambayo creator wa Tanzania ataweka kwenye Bio yake. Huu ni mfumo ambao tayari una mfumo rahisi wa malipo, unaweza kukupa creator uharaka wa kupost kazi zako na mara moja audience yako ikaanza kuzipata.

Ni muda sasa uanze kufanya content zako kuwa biashara na sio chakula tu cha algorithm ili uzidi kufaidisha wenye platforms. Ukiwa na followers 10,000 alafu 1% yao tu wakanunua bidhaa yako ya TZS 10,000 tayari umetengeneza 1,000,000. Hakuna kusubiri brand fulani ikupe ruhusu ya kupost aina hiyo ya content wapa hela kupotea kwenye fee za foreign exchange.

Platform ya kusambazia content tayari unayo. Ingia Habariduka tengeneza akaunti kisha anza kuweka bidhaa zako. 

Audience yako wani tayari kukulipa ila ni wewe hujawapa tu sehemu watatumia kukulipa.

Kama umependa andiko hili usiache kuanche comment au kunipa walau tip ya chapati moja hapo chini. Jero tu nipate chapati moja kwa mama Juma.