Kama Ningekuwa Naanza Upya Leo, Ningefanya Haya Tofauti

Kama Ningekuwa Naanza Upya Leo, Ningefanya Haya Tofauti

Nina zaidi ya miaka 14 tangu nimeanza kufanya kazi za mtandaoni, kuna vitu nilivyoamini mwanzoni ambavyo sasa naona vili nipotezea muda tu. Kama ningeanza leo, kuna vitu 5 ninge vifanya tofauti kabisa.

1. Nilidhani idea ndiyo kila kitu.

Kumbe siyo.

Idea nzuri isiyotatua tatizo la mtu ni wazo tu.

Biashara inaanza pale unapogusa tatizo ambalo watu wako tayari kulitafutia suluhisho.

Siku nilipoacha kujiuliza, "Nifanye nini?" nikaanza kujiuliza, "Watu wanahitaji nini?" mambo yakaanza kubadilika.

2. Nilikuwa nafanya kazi sana, lakini sikuwa najenga mfumo.

Nikichoka, kila kitu kilisimama.

Hapo ndipo nilipojifunza kuwa biashara haipaswi kutegemea nguvu zako kila siku.

Inapaswa kutegemea mfumo.

Mfumo ndiyo unaokupa nafasi ya kupumzika bila biashara kusimama.

3. Skill moja inaweza kukulisha.

Lakini ukijua kuziunganisha skills zako, unajitengenezea fursa.

Leo ukijua kutengeneza content, kuitangaza na kutumia AI vizuri, huhitaji kusubiri mtu akupe nafasi.

Unaanza kujitengenezea nafasi mwenyewe.

4. AI siyo uchawi.

Watu wengi wanaitarajia AI iwafanyie kazi.

Lakini ukweli ni kwamba AI inamsaidia zaidi mtu ambaye tayari anajua anachotaka.

Usipojua unakoenda, hata AI itakuzungusha.

5. Nilikuwa napima maendeleo kwa pesa niliyoingiza.

Leo napima mafanikio kwa kile nilicho kitengeneza.

Brand.

Audience.

Content.

My list.

Connections.

Hivi ndivyo vitu vinavyoendelea kukulipa hata siku ambayo hufanyi kazi.

Kadri muda unavyopita, ndivyo ninavyozidi kuelewa kuwa biashara ya mtandaoni si kitu cha kufanya siku moja.

Ni process ya kujenga kitu kitakacho kuwa na thamani hata baada ya miaka kadhaa.

Ukijenga hicho leo, kesho hutaanza tena kutoka sifuri.