Kazi za Remote Work ni UTUMWA.
Ndiyo.
Nimesema utumwa.
Lakini sio kwa sababu unafanya kazi ukiwa nyumbani.
Bali kwa sababu watu wengi wameingia kwenye remote work wakiwa na mawazo kwamba ndiyo tiketi ya uhuru wa kifedha.
Ukweli ni tofauti.
Ukitegemea client mmoja tu...
Ukitegemea platform moja tu...
Ukifanya kazi masaa 10 hadi 12 kila siku ili ulipwe mwisho wa mwezi...
Basi umebadilisha tu sehemu unayofanyia kazi.
Sio mfumo.
Bado kuna mtu anaamua unalipwa kiasi gani.
Anaamua lini akupe kazi.
Na anaweza kukuondoa wakati wowote.
Huo sio uhuru.
Ni ajira iliyovaa nguo mpya.
Usinielewe vibaya.
Remote work ni fursa kubwa sana. Nimeiona ikibadilisha maisha ya watu wengi. Mimi pia ni mmoja wapo wa watu hao.
Lakini ifanye iwe daraja, sio mwisho wa safari.
Tumia kipato unachopata kujenga assets zako.
Jenga brand yako.
Tengeneza bidhaa zako.
Jenga audience yako.
Kwa sababu siku ambayo kipato chako hakimtegemei client mmoja, ndipo utaanza kuonja uhuru wa kweli.
Remote work inaweza kuwa mwanzo wa uhuru wako. Au inaweza kuwa utumwa wa kisasa.
Tofauti ipo kwenye mfumo unaojijengea, sio sehemu unayofanyia kazi.

P.S.
Nimeona watu wengi wakifundishwa jinsi ya kupata client.
Lakini wachache sana wanafundishwa jinsi ya kuacha kumtegemea client.
Ndiyo sababu nimeandika eBook mpya inayoitwa THE INTERNET ATM.
Ndani yake sitaonyesha tu jinsi ya kutengeneza kipato mtandaoni.
Nitakuonyesha jinsi ya kujenga mfumo ambao unaendelea kukuingizia pesa, hata pale ambapo client mmoja ameondoka.
Inakuja hivi karibuni.
