Moja ya makosa makubwa ambayo creators wengi wanafanya ni kutaka kuwa original kupita kiasi.
Na mimi nilikuwa mmoja wao.
Nilikuwa naamini kila content lazima ianze na idea mpya kabisa.
Kumbe nilikuwa najiongezea ugumu usio na sababu.
Kadri nilivyoendelea kujifunza kutoka kwa creators wakubwa duniani, ndivyo nilivyogundua kitu kimoja.
Wengi wao hawajaanza kwa kubuni kitu kipya.
Wameanza kwa kuelewa ni nini tayari kinafanya kazi.
Kisha wakakiboresha.
Wakakileta kwa style yao.
Na wakakifanya kiwafae audience yao.
Hapo ndipo tofauti inaanzia.
Mfano mzuri ni Ryan Trahan.
Ukichunguza content zake kwa makini, utaona hakuvumbua kila format kutoka sifuri.
Alichukua challenge format ya Mr Beast iliyokuwa inafanya vizuri.
Akaichanganya na storytelling na vlog style ya Casey Neistat.
Matokeo yake yakawa kitu kipya ambacho watu walikipenda.
Huo ndiyo uwezo ambao creator anatakiwa kuujenga.
Siyo tu uwezo wa kubuni kila kitu. Bali uwezo wa kuona kinachofanya kazi na kukiboresha.
Kwa sababu ukweli ni huu...
Internet haiwalipi sana watu wanaolazimisha originality.
Inawalipa watu wanaoweza kuchukua idea nzuri na kuifanya iwe bora zaidi kwa audience yao.
Hata hapa Bongo unaweza kuona mfano wa mtu kama KIREDIO, na JOWZEY.. Wameona Streaming ndio zina fanya kwazi kwa sasa wakiwatazama creators kama Ishow Speed kwa kile wana kifanya na kukiboresha kuendana na mazingira ya Tanzania yalivyo na nini watu wana penda.
Ndiyo maana siku hizi sitazami niche yangu pekee.
Naangalia kila mahali.
Naweza kujifunza hook kutoka niche ya finance.
Storytelling kutoka kwenye content za travelling.
Editing style kutoka kwenye gaming.
Retention strategy kutoka kwenye documentaries.
Halafu navichanganya kwenye niche yangu.
Hapo ndipo content inaanza kuwa tofauti.
Kwa hiyo badala ya kujiuliza kila siku,
"Ni content gani mpya nifanye?"
Jaribu kujiuliza,
"Ni format gani tayari inafanya vizuri... na ninawezaje kuifanya iwe yangu?"
Mara nyingi, hapo ndipo ideas bora huanzia.
Naimani umejifunza kitu..
PS:
Kama unataka kujifunza mfumo ninaotumia kutafuta ideas, kutengeneza faceless YouTube channels, na kujenga content inayopata views bila kubahatisha... Nimefundisha kila hatua ndani ya YouTube Automation Masterclass.
Utajifunza kuanzia kutafuta niche, kutengeneza content, kutumia AI kwa usahihi, kuongeza retention, hadi kukuza channel hatua kwa hatua.
Jiunge hapa: YouTube Automation Masterclass by Ally Msangi