Pesa Haiko Kwenye Internet, Ipo Kwenye Mifuko ya Watu Wengine

Pesa Haiko Kwenye Internet, Ipo Kwenye Mifuko ya Watu Wengine

Jana nilikuwa nafikiria kuhusu kitu kimoja... Kwa nini mtu anaweza kuwa na laptop, Internet na skill nzuri, lakini bado akawa hana pesa?

Halafu mtu mwingine mwenye vitu hivyo hivyo anaweza kuanza kupata $100, $500, $1,000 au zaidi kutoka kwenye Internet?

Tofauti ipo wapi?

Nilipoanza kulifikiria zaidi, nikagundua kitu. Pesa nyingi tunazo tafuta tayari zipo.

Hazijapotea. Wala hazijafichwa.

PESA yoyote ile unayo itaka tayari ipo. Tatizo ni kwamba haipo kwenye mfuko wako. Ipo kwenye mfuko wa mtu mwingine.

Kuna mtu anataka website. Mwingine anataka logo.

Mwingine anataka content. Mwingine anataka kuuza bidhaa zake.

Na mwingine anataka kujifunza skill. Mwingine anataka kupata wateja.

Alafu kuna mwingine anataka mtu amsimamie social media zake.

PESA IPO.

Unacho takiwa ni kujiuliza swali hili tu... Je, una njia ya kuifikia?

Hapa ndipo watu wengi wanaelewa vibaya kuhusu internet. Wanafikiri ili utengeneze pesa online lazima uwe na bidhaa.

SIO LAZIMA.

Wengine wanafikiri lazima uwe na mtaji. Sio lazima.

Wengine wanafikiri lazima uwe influencer. Sio lazima.

Unachohitaji kwanza ni vitu vitatu...

SKILL + ATTENTION + TRUST.

Uwe na kitu unachoweza kufanya. Watu wajue kwamba unaweza kukifanya. Na wakuamini kiasi cha kukulipa.

Hapo ndipo THE INTERNET ATM inaanza kufanya kazi Sasa.

Ebu fikiria ATM ya kawaida tu. ATM yenyewe haina pesa yako. Inakupa access kwenye pesa iliyo kwenye account yako.

Internet nayo ni hivyo hivyo. Internet haikutengenezei pesa kwa uchawi.

Inakupa access kwa mamilioni ya watu ambao tayari wana pesa, wana matatizo, wana mahitaji, na wako tayari kulipa mtu anaye weza kuyatatua.

Ndio maana mtu mwenye laptop na skill moja anaweza kuanza kupata pesa bila kuwa na office.

Anaweza kuandika. Anaweza design. Anaweza edit video. Anaweza kutengeneza websites. Anaweza kuuza. Anaweza kufundisha. Anaweza kusimamia accounts za watu. Anaweza kutengeneza digital products. Anaweza hata kuuza bidhaa za mtu mwingine na kuchukua commission.

Hatengenezi pesa kutoka hewani tu. Anahamisha pesa kutoka kwenye mfuko wa mtu mwingine kwenda kwenye mfuko wake kwa kutoa value.

Na hapa ndipo kuna SIRI ambayo watu wengi hawajaiona...

Huhitaji kuwa na watu wengi. Unahitaji kuwa na access kwa watu SAHIHI.

Follower 100,000 ambao hawahitaji unachouza wanaweza kuwa na thamani ndogo kuliko watu 500 wanao kuhitaji.

Ndiyo maana nimeipa eBook yangu jina la "THE INTERNET ATM". Sio kwa sababu internet ni mashine ya kutoa pesa.

Bali kwa sababu ukiielewa vizuri, internet inakuwa njia yako ya kufikia watu... Huu ni mfumo.

PEOPLE → PROBLEMS → VALUE → MONEY.

Na ukishajua kutumia mfumo huo, unaanza kuacha kuuliza... "Nitawezaje kupata pesa?"

Unaanza kuuliza... "Ni nani ana tatizo ambalo ninaweza kulitatua?"

Hapo ndipo utaona mambo kwa jicho tofauti. Kwa sababu pesa nyingi hazipatikani kwa kuitafuta.

Zinapatikana kwa kutatua matatizo ya watu ambao wana uwezo wa kulipa.

Hiyo ndiyo theory ya THE INTERNET ATM.


PS: Kama Bado haujapata kitabu cha THE INTERNET ATM... BOFYA HAPA kupata copy yako.

THE INTERNET ATM