Siri ya Mafanikio Makubwa Ni FOCUS

Siri ya Mafanikio Makubwa Ni FOCUS

Leo nataka tuzungumzie kitu kimoja muhimu sana...

FOCUS.

Muda huu nimekaa kwenye coffee shop nikifanya kazi zangu, lakini kuna kitu kilichonivutia.

Kuna msichana amekaa upande wangu wa pili akiwa na laptop yake.

Kwa jinsi anavyoonekana, unaweza kudhani yuko busy sana.

Lakini nilipoangalia vizuri...

Niliona anachofanya ni kuzunguka kwenye Instagram, TikTok, WhatsApp mara kwenye Gmail na kutuma ujumbe kwenye simu yake.

Usinielewe vibaya.

Kila mtu ana namna yake ya kufanya kazi.

Lakini ilinifanya nijiulize swali moja...

Je, kweli anatumia muda wake vizuri hapa?

Tofauti na yeye, mimi ninapokuwa sehemu kama hii huwa niko kwenye hali ya kazi kwa umakini mkubwa.

Nafanya kazi zinazohitaji mawazo ya kina.

Namaliza majukumu muhimu.

Nafikiria hatua zinazofuata za kukuza biashara yangu.

Hiyo ndiyo namna ninavyofanya kazi.

Kwa sababu nimegundua kitu kimoja...

Muda ni rasilimali ambayo haiwezi kurudi.

Kwa udadisi, niliamua kuzunguka kwenye coffee shop kuangalia watu wengine walikuwa wanafanya nini.

Matokeo yalikuwa ya kushangaza.

Watu 8: Walikuwa wameingia kwenye mitandao ya kijamii na video za TikTok.

Watu 5: Walikuwa wamezama kwenye emails, WhatsApp na ujumbe mbalimbali.

Watu 0: Walikuwa wanafanya kazi ya kina yenye maana.

Hii haikuwa utafiti rasmi wa kisayansi. Lakini ilinionesha kitu cha wazi kabisa kuwa...

"Vitu vinavyo tuvuruga vipo kila mahali."

Na kila siku vina tuibia muda na umakini ambao tungeweza kutumia kujenga kitu muhimu.

Ebu fikiria kidogo.

Ni mara ngapi tunachanganya kuwa busy na kuwa productive?

Ni masaa mangapi yanapotea tukiwa tunajibu emails zisizoisha?

Ni muda gani unapotea tukiwa tunasogeza vidole kwenye social media bila sababu?

Tatizo sio kwamba hatuna muda. Mara nyingi tatizo ni kwamba muda wetu hauna mwelekeo.

Lakini kuna suluhisho rahisi kuliko tunavyofikiria.

Neno moja tu... FOCUS.

Naamini focus ndiyo siri inayo watenganisha watu wanao fanikiwa na wale wanaobaki na mipango tu.

Inawatenganisha watu wanaotekeleza na wale wanao ota ndoto.

Inawatenganisha wanaojenga maisha wanayotaka na wale wanaosubiri mazingira yabadilike.

Fikiria kama ungekusanya hata sehemu ndogo ya umakini wako uliotawanyika kila siku...

Na kuuelekeza kwenye lengo moja.

Ungeweza kujenga nini?

Ni kiasi gani ungeweza kujifunza?

Ni biashara gani ungeweza kukuza?

Hiyo ndiyo nguvu ya focus.

Bado hujaamini?

Angalia historia ya watu waliofanikiwa zaidi duniani.

Wajasiriamali. Wabunifu. Watu wanaobadilisha dunia.

Kuna kitu kimoja wanacho fanana nacho.

Wana uwezo wa kuzingatia kitu kimoja kwa muda mrefu.

Sio kwamba hawana distractions.

Ni kwamba wanajua nini kinastahili kupata muda na nguvu zao.

Hata Joseph Kusaga huwa na kauli moja tu "FOCUS, FOCUS, FOCUS" hii sio bahati mbaya.

Kwa hiyo changamoto yangu kwako ni hii... Rudisha focus yako.

Acha kutumia nguvu nyingi kwenye vitu vinavyo kupa hisia ya kufanya kazi bila matokeo.

Anza kuweka muda wa kufanya kazi ya kina.

Jenga kitu muhimu.

Jifunze skill yenye thamani.

Fanya kazi kwenye ndoto zako bila kuruhusu kila notification ikuvute pembeni.

Kwa sababu mwisho wa siku...

Mafanikio hayaji kwa kufanya kila kitu.

Yanakuja kwa kufanya vitu muhimu kwa umakini mkubwa.

FOCUS ndiyo tofauti kati ya mtu anayetamani na mtu anayefanikisha.