Kuna Siku Unakaa Kimya Tu.

Unachukua Simu Yako.

Unafungua Mitandao.

Unaanza Kuona Maisha Ya Watu Wengine.

  • Mtu Anaonyesha Gari Jipya.
  • Mwingine Anaonyesha Biashara Yake.
  • Mwingine Anaonekana Anasafiri Sehemu Nzuri.

Unatazama Kwa Dakika Chache Tu.

Lakini Ghafla Mawazo Yanaanza Kuingia Kichwani.

Unajiuliza:

"Inawezekana Nimechelewa Maishani?"

Au Unasema Kimya Kimya:

"Dah! Watu Wote Wanaonekana Wanaenda Mbele… Mimi Je?"

Dakika Chache Za Kuangalia Maisha Ya Watu Wengine…

Zinaanza Kubadilisha Kabisa Jinsi Unavyoona Maisha Yako.

Ipo Hivi Rafiki Yangu Mpendwa...

Watu Wengi Sana Wanapitia Hali Hii.

Unaanza Kujilinganisha Na:

  • Mafanikio Ya Watu Wengine
  • Hatua Za Watu Wengine
  • Maisha Ya Watu Wengine

Na Polepole Unaanza Kuhisi Kama Wewe Uko Nyuma.

Lakini Kuna Kitu Kimoja Watu Wengi Hawakioni.

Mitandao Ya Kijamii Inaonyesha tu

Sehemu Nzuri Tu Ya Maisha Ya Watu.

Unaona:

  • Ushindi Wao
  • Mafanikio Yao
  • Matokeo Yao

Lakini Hauoni:

  • Changamoto Zao
  • Makosa Yao
  • Safari Ndefu Waliyopitia

Ndiyo Maana Kujilinganisha Kunaweza

Kukufanya Uone Kama Maisha Yako Hayasongi…

Wakati Ukweli Ni Kwamba Kila Mtu Ana Safari Yake.

Sikia Sasa... Fanya Hivi 👇🏻

Badala Ya Kuangalia Maisha Ya Watu Wengine Kila Siku…

Anza Kujiuliza Swali Moja Rahisi:

“Ni Hatua Gani Ndogo Ninaweza Kuchukua Leo Kuboresha Maisha Yangu?”

Maisha Hubadilika Polepole Rafiki Yangu.

Tena...

Kwa Hatua Ndogo Ndogo.

Na Hatua Hizo Zinatokea Pale Unapolenga Safari Yako Mwenyewe,

Si Ya Mtu Mwingine.

Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:

Ukikaa Sana Ukiangalia Safari Za Wengine…

Unaweza Kusahau Kuanza Safari Yako Mwenyewe.

Lakini ...

Kuna Tabia Nyingine Moja Ya Kawaida Sana

Ambayo Inaiba Muda Wa Watu Wengi Kila Siku Bila Wao Hata Kugundua.

Kesho Nitaielezea.

Kama umesoma Mapaka hapa

Like Au Toa Reaction Yoyote

🙏🏽-🔥-👍-💪🏾

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 4

...

FRANCIS | ABRACADABRA