⚠️ Tabia Ya 5 - Tabia Ya Kusubiri Mpaka "Ujisikie" Tayari Ndipo Uanze

⚠️ Tabia Ya 5 - Tabia Ya Kusubiri Mpaka "Ujisikie" Tayari Ndipo Uanze

Kuna Watu Wengi Wana Ndoto Nzuri Sana.

Lakini Kuna Sentensi Moja Wanayoisema Mara Nyingi Sana.

"Nitaanza Nikiwa Tayari."

Wanataka:

  • Kujifunza Kila Kitu Kwanza
  • Kupanga Kila Kitu Vizuri Kwanza
  • Kujihakikishia Kila Kitu Kitafanya Kazi

Kwa Nje Inaonekana Kama Wanafanya Maandalizi.

Lakini Ukweli Ni Kwamba…

Wanasubiri Kujisikia Tayari Kabisa.

Which Is Very Bad...

Utaniuliza: "Francis Kwanin?"

Kwasababu - Hapo Ndipo Muda Unaanza Kupita.

  • Wiki Zinapita.
  • Miezi Inapita.

Mpaka Siku Moja Wanamuona Mtu Mwingine Tayari Ameanza

Kufanya Kile Walichokuwa Wanapanga.

Unaweza Hisi Kabisa Kuna Kitu Unapaswa Kuanza.

Lakini Ndani Yako Kuna Sauti Inayokuambia:

"Subiri Kidogo Kwanza."

↳ Unafikiri Bado Hujajua Vya Kutosha.

↳ Unafikiri Bado Hujajiandaa Vya Kutosha.

Na Polepole Hatua Ya Kwanza Inaendelea Kusogezwa Mbele.

Ukweli Ambao Watu Wengi Hawaujui Ni

Hakuna Mtu Anayewahi Kuhisi Kwamba Yupo Tayari Kabisa.

Watu Wengi Wanaofanikiwa Huanza Wakiwa:

  • Bado Wana Hofu
  • Bado Hawajui Kila Kitu
  • Bado Hawajajiandaa Kikamilifu

Lakini Wanaanza.

Na Wanajifunza Njiani.

Utaniuliza:

"Francis Mimi Nina Tatizo Kama Hili. "

"Nifanyeje Ili Niepukane Na Hii Tabia"

Fanya Hivi...

Badala Ya Kusubiri Ujisikie Upo Tayari Kabisa…

Anza Kwa Hatua Ndogo Sana.

Inaweza Kuwa:

  • Kujaribu Hatua Ya Kwanza
  • Kujifunza Kwa Vitendo Na Sio Kusoma Tu
  • Kuanza Kidogo Kidogo

Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:

Kuanza Ndiko Kunakokufanya Uwe Tayari.

Na Sio Kusubiri.

Hatua Ya Kwanza Inaweza Kuwa Ndogo Sana…

Lakini Ndiyo Inayoweza Kufungua Milango Mingi Baadaye.

...

Lakini Kuna Tabia Nyingine Moja

Ambayo Imezuia Watu Wengi Kuanza

Kabisa Hata Pale Wanapokuwa Na Wazo Zuri Sana.

Tabia Ya Kuogopa Kuonekana Mjinga Au Kushindwa.

Kesho Nitaielezea Stay Tune

Kama Umesoma Mapaka Hapa

Like Au Toa Reaction Yoyote

-🔥-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 6

...

FRANCIS | ABRACADABRA