😭 TABIA YA 6 - Tabia Ya Kuogopa Kuonekana Mjinga Au Kushindwa

😭 TABIA YA 6 - Tabia Ya Kuogopa Kuonekana Mjinga Au Kushindwa

Kabla Sijaendelea Kwenye Tabia Hii

Ambayo Imekuwa Ni Ugonjwa

Sugu Kati Ya Watu Wengi.

Naomba Kama Bado Hujasoma Tabia 5

Ambazo Tayari Zipo Hapo Juu

Naomba Uzisome Na Pengine Zikakusaidia Kujua

Wapi Inabidi Urekebishe ...

Ok... Tuendelee

Sasa Leo Tupo Kwenye Tabia Ya 6

Imagine Labda Unataka Kuanza

Biashara Mpya.

Project Mpya.

Content Creation

Au Ujifunze Skill Mpya.

Lakini Kabla Hata Haujaanza…

Akili Inaanza Kukuletea Maswali.

  • Itakuwaje Kama Nikishindwa?
  • Itakuwaje Kama Watu Watanicheka?
  • Itakuwaje Kama Nitaonekana Sijui Ninachofanya?

Na Ghafla Unaamua Kitu Kimoja.

Kuacha Kabisa Kujaribu.

Si Kwa Sababu Wazo Halikuwa Zuri.

Bali Kwa Sababu Anaogopa Kuonekana Mjinga Mwanzoni.

Hii Ni Hali Ambayo Karibu Kila Mtu Amewahi Kupitia.

Unataka Kuanza Kitu Fulani.

Lakini Ndani Yako Kuna Sauti Inakuambia:

"Watu Watasema Nini?"

Unaanza Kuwaza:

  • Maoni Ya Watu
  • Kuchekwa Na Wengine
  • Kushindwa Mbele Ya Watu

Na Polepole Wazo Zuri Linaishia Kubaki Kichwani.

Utaniuliza: Francis - Kivipi Hofu Hii Inazuia Watu Wengi Sana?

Sababu Ni Moja Tu...

Watu Wengi Wanataka Kuonekana

Wako Vizuri Tangu Mwanzo.

Lakini Ukweli Wa Maisha Hauko Hivyo.

Kila Mtu Anayeanza Kitu Kipya Hupitia Hatua Hii:

• Kufanya Makosa Mwanzoni

• Kujifunza Polepole

• Kuonekana Hajui Kila Kitu

Kwa Kifupi…

Mwanzoni Kila Mtu Anaonekana Mjinga Kidogo.

Lakini Tofauti Ni Moja.

Wengine Wanaendelea.

Wengine Wanaacha Kabla Hata Hawajaanza.

Kama Ukiniuliza "Nawezaje Kupukana Na Hali/Tabia Hii?"

Nitakwambia Kwamba -

Kama Unataka Kusonga Mbele Maishani…

Lazima Ukubali Ukweli Mmoja Rahisi.

Hatua Za Mwanzo Hazitakuwa Perfect.

Na Hilo Ni Kawaida Kwa Watu Wote.

Badala Ya Kuogopa Kuonekana Hujui Kila Kitu…

Anza Kujifunza Kwa Vitendo.

• Jaribu

• Fanya Makosa

• Rekebisha Ukiwa Unaendelea Kusonga

Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:

Watu Wanaofanikiwa Si Wale Ambao

Hawajawahi Kuonekana Wajinga.

Ni Wale Ambao Hawakuogopa Kuanza.

Lakini Kuna Tabia Nyingine Moja Ambayo Imepoteza

Fursa Nyingi Sana Kwa Watu Wengi.

Tabia Ya Kuahirisha Maamuzi Muhimu.

Na Mara Nyingi Mtu Anapogundua Kosa Hilo…

Fursa Tayari Imepita.

Baadae Nitaielezea - Stay Tune

Kama Umesoma Mapaka Hapa

Like Au Toa Reaction Yoyote

-🔥-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌 - ❤️

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 7

...

FRANCIS | ABRACADABRA