🚨 TABIA YA 7 - Tabia Ya Kuahirisha Maamuzi Muhimu

🚨 TABIA YA 7 - Tabia Ya Kuahirisha Maamuzi Muhimu

Kuna Muda Maisha Yanakuletea Fursa.

Sio Kubwa Sana Kwa Macho Ya Nje…

Lakini Ndani Unajua Kabisa:

"Hiki Kitu Kinaweza Kubadilisha Mwelekeo Wa Maisha Yangu."

Unakaa Chini.

Unaanza Kufikiria.

  • Unaona Faida Zake.
  • Unaona Hasara Zake.
  • Unaanza Kupima Kila Kitu.

Mwisho Unasema:

"Ngoja Nifikirie Kidogo Kwanza."

Siku Inapita.

Wiki Inapita.

Bado Hujachukua Hatua.

Mpaka Siku Moja Unakuja Kugundua…

Ile Fursa Haipo Tena.

Labda Mtu Mwingine Tayari Ameichukua.

Au Mazingira Yamebadilika.

Na Hapo Unasema Kwa Huzuni: 😭

"Nilikuwa Karibu Sana Kuanza..."

Watu Wengi Sana Wamewahi Kupitia Hali Hii.

Unajua Kabisa Kuna Uamuzi Unatakiwa Kufanya.

Lakini Badala Ya Kuamua…

Unaendelea Kuusogeza Mbele.

  1. Unaogopa Kufanya Kosa.
  2. Unaogopa Kujuta.
  3. Unaogopa Kuchagua Upande Usio Sahihi.

Na Polepole Muda Unapita…

Bila Maamuzi Kufanyika.

Utaniuliza...

"Francis, Kwa Nini Watu Wengi Wanaahirisha Maamuzi Muhimu?"

Kwa Sababu Wanatafuta Kitu Kisichokuwepo.

Uhakika Wa 100% Ya Watu.

Wanataka Wajue Kila Kitu

Kitaenda Sawa Kabla Hawajaamua.

Lakini Ukweli Ni Huu:

Maamuzi Mengi Makubwa

Maishani Hayaji Na Uhakika Kamili.

Yanahitaji Uamuzi, Kisha Hatua.

Na Kadri Unavyoahirisha Maamuzi…

Ndivyo Unavyopoteza:

• Muda

• Fursa

• Mwelekeo Wa Maisha Yako

Ufanyaje Sasa Kama Tabia Hii Imekuwa

Ikikutesa Kwa Muda Mrefu...

Nakupa Hatua Hizi Ndogo Ambazo Zitakusaidia

Listen... My Friend

Kama Unataka Kusonga Mbele…

Jifunze Kufanya Maamuzi Kwa Wakati.

Sio Lazima Ujue Kila Kitu.

Unachohitaji Ni:

  • Taarifa Za Msingi
  • Uelewa Wa Hatua Ya Kwanza
  • Uamuzi Wa Kuanza

📍Kumbuka Hili:

Ni Bora Kufanya Uamuzi Usio Perfect Kuliko Kutokufanya Uamuzi Kabisa.

Kwa Sababu Maisha Hubadilika Pale Unapochagua Mwelekeo…

Sio Pale Unapobaki Ukifikiria Tu.

Lakini Kuna Tabia Nyingine Moja

Ambayo Inawafanya Watu Wengi

Washindwe Kudumu Kwenye Kile Wanachoanza.

Wanasubiri Kitu Fulani Kihamasishe…

Na Bila Hicho, Kila Kitu Kinasimama.

Kesho Nitaielezea.

Kama Umesoma Mapaka Hapa

Like Au Toa Reaction Yoyote

-🔥-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌 - ❤️

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 7

...

FRANCIS | ABRACADABRA