⚠️ Tabia Ya 9 - Tabia Ya Kufikiria Sana Kuliko Kuchukua Hatua

⚠️ Tabia Ya 9 - Tabia Ya Kufikiria Sana Kuliko Kuchukua Hatua

Kuna Watu Wana Akili Sana.

↳ Wanafikiria Kwa Kina.

↳ Wanapanga Vizuri.

↳ Wana Idea Nyingi.

Kila Wanapotaka Kuanza Kitu…

Wanaanza Na Kufanya Research.

  • Wanasoma.
  • Wanaangalia Videos.
  • Wanauliza Watu.

Siku Zinaenda.

Wiki Zinaenda.

Wanaendelea Kujifunza Zaidi Na Zaidi.

Lakini Kuna Kitu Kimoja Hakifanyiki.

Hawaanzi.

Wanasema:

"Ngoja Nijue Vizuri Kwanza."

"Ngoja Nijipange Vizuri Zaidi."

Mpaka Siku Moja Wanamuona Mtu Mwingine…

Ameanza Tayari.

Na Si Perfect.

Lakini Yuko Mbele Yao.

Na Hapo Wanabaki Na Sentensi Moja:

" Dah 😭 Ningekuwa Nimeanza Mapema…"

Hii Ni Hali Inayowapata Watu Wengi Sana.

Inawezekana Pia Wewe Ni Mmoja Wapo

Unayesoma Hapa ...

Unajua Kabisa Unataka Kufanya Kitu.

Lakini Unajikuta Uko Kwenye Duara La;

  • Kufikiria Sana
  • Kupanga Sana
  • Kujifunza Sana

Lakini Hatua Halisi Ni Ndogo Sana… Au Hakuna Kabisa.

Na Ndani Yako Unajua:

Unaweza Kufanya Zaidi Ya Hapo.

Utaniuliza:

Francis, Kwa Nini Kufikiria Sana Kunakuwa Tatizo?

Sababu Ni Kuwa

Kufikiria Sana Wakati Mwingine

Kunakupa Hisia Ya Uongo.

Unahisi Kama Unasonga Mbele…

Wakati Ukweli Ni Kwamba Bado Hujaanza.

Kufikiria Ni Muhimu.

Lakini Kufikiria Kupita Kiasi Kunageuka Kuwa:

• Kuchelewesha Hatua

• Kuongeza Hofu

• Kupunguza Ujasiri

Na Kadri Unavyoendelea Kufikiria…

Ndivyo Kuanza Kunavyozidi Kuwa Kugumu.

Ok..Ngoja Nikupe Mbinu Hii Bure

Ambayo Huwa Naitumia Na Imeleta Matokea

99% Ya Kufanikisha Kuanza Na Kuendelea

Bila Kuwaza/Kufikiria Sana...

Fanya Hivi....

Badala Ya Kusubiri Ujue Kila Kitu…

Anza Na Kile Unachokijua Sasa.

Chukua Hatua Ndogo Tu.

• Anza Kabla Haujajua Kila Kitu

• Jifunze Kupitia Kufanya

• Rekebisha Ukiwa Njiani

Na Hili Nimekuwa Nikilisisitiza Kila Mara

Kwenye Madini Yangu Yote Ninayoweka

Humu... Ngoja Nirudie

Chukua Hatua Ndogo Tu... Alafu

Anza Taratibu Huku Ukitengeneza

Mfumo Utakaokusaidia Kufanya

Hata Kama Hujisikii..

Nimesema Hili Ndani Ya Tabia Ya 8

📍Kumbuka:

Hatua Ndogo Leo Ina Thamani Zaidi Kuliko Mipango Mikubwa Kichwani.

Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:

Maisha Hubadilika Kwa Kufanya…

Sio Kwa Kufikiria Tu.

Lakini...

Kuna Tabia Ya Mwisho Ambayo Watu Wengi Huipuuza Sana…

Wakati Ndiyo Inayoweza Kubadilisha Mwelekeo Wa Maisha Yao Kabisa.

Tabia Ya Kupuuza Sauti Ya Ndani.

Baadae Nitaielezea.

Like Au Toa Reaction Yoyote

-🚨-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌 - 💔

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya Mwisho (10)

...

FRANCIS | ABRACADABRA