Kuna mambo mengi sana yanaongelewa juu ya Artificial Intelligence. Kuna mengi ya kweli na mengi ni nadharia tu na uongo kwa sababu ya ujuaji. Kuna yale tumeona kwenye filamu ambazo ni nadharia dhania juu ya nini kinaweza tokea. Waongozaji na waandishi wa filamu wanakaa na kufikiria kipi kitavutia watazamaji wa filamu zao.
Ndipo wanakaa mezani na kuandaa hizo filamu. Sio kila unachokiona ni uhalisia wa mambo. Binadamu akili zetu siku zote zimekaa kutafuta mabaya ya kitu kwanza ndipo tuanze kuangalia mazuri yake. Na kama ilivyo kwa mambo mengine yote, Artificial Intelligence (Akili bandia) pia ina mazuri na mabaya yake.
Hayo yote ni mambo hatuwezi kuyazungumzia bila kuanza kuelewa kwanza Akili bandia ni nini na inafanya vipi kazi. Nitaongelea nikiweka akilini maswali mengi tunayojiuliza juu ya akili bandia. Maswali juu ya ajira zetu, maisha yetu, usalama wetu, faragha yetu na hata serikali zetu. Leo tunaondoa utata wote wa Akili Bandia.
Reviews
There are no reviews yet.