Arbitrage trading ni mbinu ya kununua bidhaa au mali fulani kwa bei ya chini kwenye soko moja kisha kuiuza kwa bei ya juu kwenye soko lingine na kupata faida bila hatari kubwa. Hii inatumika sana kwenye masoko ya hisa, forex, na cryptocurrency.
Mfano, kama Bitcoin inauzwa Tsh. 100 milioni kwenye exchange moja lakini Tsh. 101 milioni kwenye exchange nyingine, unaweza kuinunua kwa bei ya chini na kuiuza kwa bei ya juu mara moja na kutengeneza faida ya Tsh. 1 milioni (ukitoa makato na gharama za miamala).
Ingawa arbitrage inaonekana kama njia rahisi ya kutengeneza pesa, inakuja na changamoto kama ucheleweshaji wa miamala, makato makubwa, na mabadiliko ya bei yanayotokea haraka. Wale wanaofaulu kutumia mbinu hii hutumia mifumo ya kiotomatiki na zana za kisasa kufanikisha biashara kwa kasi.
Reviews
There are no reviews yet.