Huu Ni Ushauri Bora Sana Ambao Natamani Ningeupata Kabla Sijaingia Kwenye Safari Yangu Ya Content Creation.
Kuna kitu watu wengi hawapendi kukisikia, kujenga skills au brand mtandaoni si kitu cha siku chache. Mara nyingi unahitaji miezi sita hadi mwaka mzima wa kuhaso kabla hujaanza kuona matokeo ya maana unayoyataka. Na katika kipindi hicho lazima uwe umejipanga kwenye kimfuko. Njaa isiwe kikwazo kwako na stress zisikukatishe tamaa mapema.
Kwa sababu ukianza safari ya content creation ukiwa huna backup, kila siku utakuwa unacheza na presha. Utachoka mapema. Utataka matokeo ya haraka kwa kazi ambayo inahitaji miezi kadhaa ili ikamilike. Na hapo ndipo wengi hukata tamaa kabla hata hawajafika popote.
Ndiyo maana ni muhimu sana kuanza ukiwa na namna nyingine ya kusurvive. Iwe unaishi kwenu, kwa ndugu au uwe una side income yoyote ya kukusukuma mbele. Si kwa sababu unaogopa kushindwa bali kwa sababu unajipa nafasi ya kustahimili mchakato na kupunguza presha za njaa.
Na jambo jingine la muhimu sana: usitegemee platform pekee ikulipe.
Hili ni kosa kubwa ambalo creators wengi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunafanya. Wanajenga audience, wanapata views wengi, wanapata likes za kutosha tu alafu wanadhani pesa itaingia automatically kwa sababu tu content imeenda vizuri. Lakini ukweli ni kwamba kwenye hizi platform, geo-location zetu zinatubana. Payout ni ndogo. Monetization baadhi ya sehemu haiko sawa na hata ikiwepo haitoshi kumtoa mtu kutoka kwenye maisha ya kubangaiza. Chukulia mfano haya maokoto ya Elon kule X ππ. Elon anawafanya watu wa africa hususani watanzania kuwa kama watumwa, maokoto ili uyapate lazima ujinyime usingize uamke usiku uwe unaengage na wazungu nk...
Ndiyo maana unapaswa kufocus kwanza kwenye kumonetize kupitia skills zako na si kusubiria platform ikulipe kama mshahara. Tumia content kama mlango wa kuonyesha thamani yako. Tumia content kuvuta wateja. Tumia content kuuza huduma zako, bidhaa zako, ujuzi unaoujua au kwa opportunities nyingine. Usikae ukitegemea views za youtube na tiktok kama chanzo cha maisha yako.
Na hapa ndipo wengi wanapoangukia, wanajenga content bila mfumo wa pesa. Wanajenga audience bila direction. Wanajenga jina bila plan ya biashara. Matokeo yake wanaonekana kuwa busy sana online lakini ndani yao wako broke vibaya sana. Usibishe hii ni factππ
KAMA UNA MUDA SOMA HII ARTICLE UTANISHUKURU: https://x.com/ArthurGeil/status/2047591786298613780?s=20
Kama unataka kuwa content creator wa kweli, especially hapa Tanzania, jifunze mambo haya mapema: tengeneza backup ya maisha yako, jifunze skill inayoweza kuuzwa, jua namna ya kuuza kupitia content na usifanye kazi kwa matumaini ya kulipwa na platform tu.
Kwa kifupi, content creation si matatizo ya kupiga story na kuonekana tu. Ni safari ya uvumilivu, nidhamu na akili ya biashara. Ukizipanga vizuri, inaweza kukupeleka mbali. Ukizipuuza, itakuacha na views tu bila maisha yako kubadilika.
CHUKUA HIZI ZAWADI ZANGU KWAKO KAMA UPO SERIOUS NA CONTENT CREATION!π
1. LEARN NEW SKILLS:
Kuna vitu vingi sana vya kujifunza na sio kupoteza muda kwenye Betting, TikTok, Instagram (Mitandaoni) n.k.
Jifunze jinsi ya kutunza Pesa zako (Money management skills), Coding, Njia za kutengeneza Pesa (Money making skills), Kuwasiliana na watu (Communication skills), Biashara (Mf: Stock Markets, Hati Fungani, Kilimo, Ufugaji n.k)
Chukua Hii Free Guide!
Be Your Own Boss ( Mwongozo Wa Kujenga Uhuru Wa Muda Na Pesa)
Idownload For Free Kabisa Hapa: https://duka.habaritechnology.com/book.php?slug=be-your-own-boss
2. Usikose hiiβ¦π°
Hii eBook ni mwongozo wa vitendo wa jinsi ya kuanza freelancing na kuingiza pesa mtandaoni bila kuchanganyikiwa yani unaanza from Beginner to Pro.
Ndiyo, hata kama huna uzoefu, hata kama hujui pa kuanzia, bado unaweza kuanza kujiajiri na kujenga kipato chako kupitia mtandao.
Hii si nadharia β ni mfumo halisi wa hatua kwa hatua unaokuonyesha nini cha kufanya tangu siku ya kwanza.
π βJINSI YA KUANZA FREELANCING (HATUA 10 ZA UHAKIKA)β
Ndani yake utajifunza:
Jinsi ya kuchagua ujuzi unaolipa haraka
Jinsi ya kuanza hata kama hujui chochote
Jinsi ya kutengeneza portfolio itakayokuletea wateja
Jinsi ya kupata wateja wako wa kwanza bila connection
Jinsi ya kujiuza na kujitofautisha kwenye ushindani
Makosa makubwa ambayo wanaoanza hufanya (na jinsi ya kuyaepuka)
Hii ndio njia ambayo watu wanatumia leo kujiajiri na kuingiza kipato kupitia internet.
Ukiielewa hii, unaacha kubahatisha β unaanza kuwa na direction.
π Anza sasa safari yako ya freelancing. Mtandao unaweza kukulipa.
Hii hapa: https://duka.habaritechnology.com/book.php?slug=the-freelance-blueprint
3. Chukua Hii eBook Ya MONETIZE YOUR PERSONAL BRAND! Ikiwa unataka kujenga Profitable Personnal Brand.
https://duka.habaritechnology.com/book.php?slug=monetize-your-personal-brand-2
END.
Mwandishi: MWANAHISABATI @ArthurGeil Kutoka X