Siku Moja Unakaa Peke Yako…

Wazo Linakuja Ghafla Kichwani.

Unasisimka.

Unasema:

"Hiki Kitu Kinaweza Kufanya Kazi."

Lakini Dakika Chache Baadaye Unajisemea Kitu Kimoja Tu:

“Ngoja Nifanye Baadaye Kidogo.”

Siku Inapita.

Kesho Inakuja.

Unasema Tena:

Ngoja Nianze Wiki Ijayo.

Wiki Inapita.

Mwezi Unapita.

Mpaka Siku Moja Unafungua Simu Yako…

Unaona Mtu Mwingine Tayari Anafanya Kile Kile Kitu Ulichowahi Kuwaza.

Unakaa Kimya Kidogo.

Halafu Unasema:

"Hiki Kitu Nilifikiria Zamani Sana..."

Hii Ni Hali Inayowapata Watu Wengi Sana.

↳ Si Kwa Sababu Hawana Akili.

↳ Si Kwa Sababu Hawana Uwezo.

Bali Kwa Sababu Kuna Tabia Ndogo Sana

Ambayo Inachelewesha Hatua Zao.

Tabia Ya Kusema:

“Nitafanya Baadaye.”

Na Polepole Ndoto Nyingi Zinaishia Kubaki Kichwani.

Utaniuliza: Francis Kwanini Unasema Haya Yote.

Unajua...

Kuna Watu Wengi Wana Mawazo Mazuri Sana.

  • Wazo La Kuanza Biashara.
  • Wazo La Kujifunza Kitu Kipya.
  • Wazo La Kufanya Jambo Litakalobadilisha Maisha Yao.

Ipo Hivi...

Maisha Hayachelewi Kwa Sababu Watu Hawana Mawazo Mazuri.

Maisha Yanachelewa Kwa Sababu Hatua Ya Kwanza Inasogezwa Mbele Kila Mara.

Na Kadri Unavyozoea Kusema “Baadaye”

Ndivyo Muda Unavyoanza Kupita Bila Wewe Kugundua.

Badala Ya Kusema:

"Nitaanza Kesho."

Jaribu Kubadilisha Kitu Kimoja Tu.

Ukifikiria Kufanya Kitu…

Anza Na Hatua Ndogo Sana Siku Hiyo Hiyo.

Inaweza Kuwa:

• Kufanya Research Kidogo

• Kuandika Mpango Wako

• Kuanza Kujifunza Hatua Ya Kwanza

Hatua Ndogo Leo…

Ina Nguvu Zaidi Kuliko

Mipango Mikubwa Ya Kesho.

Kama umesoma Maka hapa

Like Au Toa Reaction Yoyote

🙏🏽🔥👍

Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya Pili

...

FRANCIS | ABRACADABRA