
Jinsi ya kufungua account.
Kama unatumia simu au laptop nenda kwenye browser yako (Chrome, Safari au nyingine tu)
Type: https://duka.habaritechnology.com/

Ikifunguka utakutana na page na namna hii...
Kama una account utabonyeza sehemu ya login na kama huna utabonyeza sign Up.
Tu assume hauna account then umebonyeza Sign Up...
Fata hizi hatua ili kufungua account...

Weka jina email kila kitu kama wanavyokuomba hapo...
Ukimaliza utapelekwa kwenye ukurasa wa login ili ujiunge kupitia password yako...

Baada ya kumaliza kulogin utapelekwa kwenye sehemu ya dashboard ambapo utafanya verification ya ID, email yako pamoja na namba ya simu ambayo itakua inapokea pesa pia unaweza kuset account ya bank ikawa inapokea pesa hakuna shida yoyote.
Baada ya kulogin utafikia sehemu kama hii...

Hapo mnaona order za watu walionunua eBooks zangu kwenye ubazi wa kulia!
Huku kwenye ubazi wa kushoto ndio kwenye dashboard ambapo utafanya verification ya email na namba ya simu pamoja ya kitambulisho chako, iwe nida au passport utakavyotaka wewe.
Okay tuseme umemaliza kila kitu! sasa na wewe unataka kuingia kwenye affiliate program za habariduka unafanyeje, sasa twende kazi...
Ukiwa hapa kwenye dashboard...

Utabonyeza hapo juu kwenye neno HABARIDUKA
Itakuleta hadi kwenye huu ukurasa rasmi wa HABARIDUKA https://duka.habaritechnology.com/
Utaona kitu kama hiki....

Na... ukiendelea kuscroll utaona product zote ambazo zimekuwa uploaded na pro creators wengine.
Mfano angalia hizi zote...

...

Hapo kuna eBooks, Articles, Stories yani courses zote za kidigitali.
Kuna ambazo zipo Free Na Nyingine Ambazo ni za kulipia.
Sasa ushaelewa jinsi gani HABARIDUKA ilivyo na inafanyaje kazi.
Twende Kwenye Ishu Yetu Iliyotuleta hapa.
AFFILLIATE PROGRAM YA HABARI DUKA INAFANYAJE KAZI??
Ipo hivi..., Creator akiwa anaupload product yake hua anaweka Affilliate commission kwenye kila product yake. Sio lazima kuiweka ila ni uzuri wake ni kwamba hua ni nzuri kwa sababu unaweza kuweka product nzuri na ukaipangia commission yenye kuvutia creators wengine alafu wao wakaichukua na kuamua kuisambaza kwa audience wao na wakapata kujiingizia kipato na wewe ukapata cha kwako.
Mimi binafsi kila product yangu hua naiwekea Commission ya 40% yes 40% ni nzuri na yenye kuvutia ikiwa utasambaza moja kazi ya product zangu na zikauzwa basi utajipatia faida iliyokua nono sana.
Karibu Dukani Kwangu Hapa: https://duka.habaritechnology.com/mwanahisabati
Chagua product moja! Narecommand uchukue hii: JINSI YA KUJENGA NA KUMONETIZE PERSONAL BRAND YAKO MTANDAONI
Utaniuliza kwanini? kwa sababu ina Bei nzuri! 15,000 Tsh
Kwa commission ya 40% ukipata mteja mmoja:
Wewe unapata Tsh 6,000 Mimi napata 9,000 Tsh.
Ukipata wateja wa 3 unakua umepata Tsh 18,000 na hapo unakua umepata Hela ya kurudi kuinunua Hii eBook kwa 15,000 na unabaki na 3000 zako kama chenchi.
Simple Tu.
Sasa ukitaka Kujoin Affilliate program utabonyeza wapi??
Twende sawa hapa:
Ukiwa umeshakwisha kuichagua hii eBook ya JINSI YA KUJENGA NA KUMONETIZE PERSONAL BRAND YAKO MTANDAONI
Namaanisha ukiwa hapa...

Kuna sehemu unaona imeandikwa Promote this ebook & Earn na kwa chini yake kuna neno Join our Affilliate program okay??
Sasa bonyeza hapo kwenye neno Join our Affilliate program
Yani hapa...

Baada ya kubonyeza hapo automatically itakuleta hapa...

Utaniuliza kwanini umeficha hapo kuna nini??
Well, hapo sehemu ya kwanza nimeficha pesa ambazo nishawahi kuingiziza kupitia bidhaa za watu wengine na conversion rate kwa sababu hayo ni ya kwangu mim na sio ya kwako. Hahahahah,....
Hiyo ni sehemu ya affilliate program yangu!
Wewe hapo kila sehemu yako itakua inaonesha 0 kwa sababu hujawahi kufanya hivo hapo nyuma kabla...
Ile sehemu ya link clicks ni namba inayoonesha link yako ya affilliate program watu wameitembelea mara ngara ngapi!
Wewe ukifika hapo kwa ubazi wa chini utaona hii...

Link ya kwanza huku ubazi wa kushoto itakua ni referral link yako wewe ya affilliate program ya account yako.
Alafu kuna link nyingine huku kwenye ubazi wa kulia hiyo ambayo hapo juu yake kuna Jina ya eBook yangu ile ya jinsi ya kujenga pro personal brand.
Then utaicopy hiyo link ya ubazi wa kulia alafu uanze kuisambaza! Ukipata mteja wewe unapata 40% zako na mimi nakula 60% zangu.
Simple tu. Yani unapata pesa bila kuhaso kutengeneza product yoyote.
Unaweza pia kuchagua product nyingine kwa kufanya hivi...

Bonyeza hiyo sehemu ya Select product uchague product zenye commission nzuri!
Kuna Be Your Own Boss Ya kwangu ina 40% pia na nyingine nyingi tu.
NB. Na recommand uchukue ile ya Jinsi Ya Kutengeneza Profitable Personal Brand yangu ndio nzuri na utapata faida nzuri!
Link yake hii hapa: https://duka.habaritechnology.com/mwanahisabati/monetize-your-personal-brand-2
Ukifanikiwa kupata chochote kit unaweza kunitip hapa: nisapoti.com/mwanahisabati
Mungu akubariki kwenye harakati zako.